dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 28, 2019

Nape Nnauye aeleza jambo hili ni uzushi!


Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema habari iliyorushwa na kituo kimoja cha runinga nchini na kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha wananchi wakilalamikia kero ya maji katika kijiji chao kuwa ni uzushi wa ajabu sana.

Nape amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter akijibu hoja iliyotolewa na mtumiaji mmoja wa mtandao huo ambaye alidai kuwa kuna watanzania katika Jimbo la Mtama (Lindi) wanakunywa na kupikia maji ambayo yanaoekana kuwa sio safi wala salama.
Baada ya madai hayo ndipo Nape ameibuka na kuandika kuwa, "Niliwaza mwanzo kunyamazia hii habari lakini nadhani haitakuwa sawa maana uongo usipojibiwa unaaminiwa! Mimi ni mkaazi wa Kijiji hiki, wiki kadhaa zilizopita nilikuwa hapa, tutafuteni mengine ya kusema badala ya kujifichia kwenye hili si sawa! Huu ni uzushi wa ajabu sana!"

Aidha Nape amekwenda mbali zaidi na kuuliza kuwa kwanini habari iliyorushwa na kituo hicho cha runinga haikuzingatia msingi wa midhania kwa kuwahoji watu wenye dhamana na suala hilo kama vile Mbunge.

Mbunge huyo ametetea zaidi kuwa ni jambo lisiloingia akilini kwamba kisima kilichoonekana kufurika wananchi wakigombea maji, ambayo si salama kuwa ndio chanzo pekee cha maji kwenye kijiji chenye zaidi ya miaka 30.

Muwakilishi huyo amekiri kuwepo kwa kero kubwa ya upatikanaji maji ingawa amedai kuwa isitiwe chumvi.

"Kama kungekuwa na shida ya kufikia hapa, nina sababu gani ya kuficha? Ninapata nini? Jimbo la Mtama kati ya mwaka 2015 na 2019 tumeshatumia zaidi ya shilingi 3.8 billion kwasababu ya maji tu. Shida haijaisha lakini tusiweke chumvi," ameandika Mbunge huyo.

No comments :

Post a Comment