Profesa Anna Tibaijuka amesema atarejesha Tsh. Bilioni 1.6 za mgao wa Rugemarila, anayetuhumiwa kwa uhujumu uchumi ili aweze kutoka mahabusu.
Mbunge huyo wa Muleba Kusini (CCM), amesema uongozi wa Shule yake ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha hizo za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara huo ili kumsaidia kutoka gerezani.
Amesema kutokana na Rais wa Tanzania, John Magufuli kushauri watuhumiwa wa uhujumi uchumi waandike barua kukiri na kurejesha fedha na mali, wao watarejesha kiasi walichopewa na Rugemarila.
“Msamaha wa Rais unapotoka ni fursa adimu, sasa fursa ukiichezea utabaki kujuta mwenyewe, kwa upande wangu na shule, sisi tunashughulika na ule mchango tulioupokea tunaurudisha mezani” ameiambia AZAM TV.
Pia amesisitiza kuwa suala hilo sio lake binafsi maana fedha hizo ni za shule, huku akieleza kuwa mwenyekiti wake (wenyekiti wa bodi), Salmon Odunga na mwenyekiti wa wazazi, Dk Kiharuzi wamekaa kwenye kikao wakaamua fedha hizo zirudi.

No comments :
Post a Comment