dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 27, 2019

TFF na ZFF wanatarajia kukutana kumaliza sintofahamu yao!

Baada ya kuibuka kwa taarifa juu ya  Shirikisho la Soka la visiwani  Zanzibar (ZFF) kuvunja rasmi Mahusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Uongozi wa shirikisho hilo umekuja na kusema kuwa kwa sasa mahusinano yao yako vizuri  na wanatarajia kukutana ili kutatua changamoto zilizojitokeza kati yao.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa wa Raisi ya ZFF Adam Natepe alisema tarifa zilizotoka Jana kwa baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii juu ya kusitisha mahusiano yao kati ya ZFF na TFF  ni ya kweli ambapo kutokana na jambo hilo TFF imeitaka ZFF kukaa pamoja na kuyamaliza,ilikuondoa mzozano huo.
Alisema Shirikisho la soka Zanzibar  ZFF limekubaliana na taarifa hiyo ambayo ilitolewa na shirikisho la  soka Tanzania Bara TFF kukaa kikao cha pamoja na kuyamaliza  mambo ambayo yaliotokea.

Alisema kweli walitoa tarifa ya kusitisha uhusiano kwa muda na ZFF lakini kwa sasa kauli  hiyo imepungua uzito kidgogo hadi pale kikao kitakapo fanyika na kuyamalizika.
Aidha alisema ZFF haina tatizo na TFF lakini kwa hatua waliofikia TFF walizalimika kusitisha  uhusiano na kwa hilo   wamekubaliana kuyamaliza ambapo ndani ya wiki inayofata kikao hicho kitafanyika.

“Hatujui wapi kitafanyika kikao hicho,lakini tumetakiwa kuwa wiki inayokuja kkitafanyika ili kumaliziana”alisema Natepe.
Upande mwengine  alisema TFF  imeiambia ZFF  kuwa agizo lao limekubalika juu ya timu za Tanzania bara ambazo hazijalipa deni lao ZFF juu wachezaji waliosajili Zanzibar ambapo TFF imesema  imetoa muda kwa timu hizo ili kullipa madeni yao.

Kikao kati ya ZFF na TFF kinatarajiwa  kufanyika muda wowote  ikiwa Zanzibar au Tanzania  na kikao hicho ndio kitaamua juu ya kuendelea  uhusiano wao kati ya pande  mbili.

No comments :

Post a Comment