dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 27, 2019

Usichokijua kuhusu ndege mpya iliyopokelewa leo na Rais Magufuli!


Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 26 ameongoza Watanzania kupokea ndege ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Ndege hii mpya imesajiliwa kwa usajili namba 5H-TCJ na imepewa 'Brand Name' ya RUBONDO ISLAND, visiwa vilivyopo mkoani Mwanza. Visiwa hivyo vina ukubwa wa kilometa za mraba 456.8, vikishabihiana na ukubwa wa Manispaa ya Kinondoni iliyopo Dar es Salaam.
Ndege mpya ya Air Tanzania, Boeing 787-8 ina uwezo  wa kutembea kilometa 13620 sawa na saa zaidi ya 12 hewani bila ya kusimama. Inabeba lita 101,000 za mafuta na ina ukubwa wa mita 56.72, yaani ni sawa na nusu ya Uwanja wa Mpira wa Miguu.

Boeing 787-8 inabeba jumla ya abiria 262, ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 227 yaani 227,930Kg wakati wa kupaa, uzito huo hujumuisha uzito wa chombo, mizigo na mafuta. Inapotua Inatakiwa iwe na tani  172 za uzito kutokana na kupungua kwa kiasi cha mafuta.

Sifa nyingine kubwa ya ndege hii ina uwezo mkubwa wa kuhimili hali nzito ya hewa, ikiwa kwenye umbali mrefu kwenda juu.

No comments :

Post a Comment