Baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa CAG, Charles Kichere amemshukuru Rais kwa kumuamini kushika nafasi hiyo, huku pia akiweka wazi kuwa atahakikisha anazidisha mahusiano mazuri baina ya ofisi ya CAG na Bunge la Tanzania ili kuisimamia Serikali.
Kichere ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV iliyotaka kufahamu neno lake baada ya kuteuliwa.
"Kwanza namshukuru Rais kwa kuniteua kuwa CAG, la pili ni kwenda kuungana na wenzangu wa ofisi ya CAG tufanye kazi zetu kwa uadilifu mkubwa, ili kuhakikisha pesa za Serikali zinatumika kama zilivopangwa" amesema Kichere.
"Kuhusiana na ushirikiano baina ya mtangulizi wangu Musa Assad na Bunge, siamini kama yalikuwa ni hafifu kwasababu Kamati za PAC zilikuwa zikifanyia kazi taarifa zake, labda cha muhimu ni kuzidisha uhusiano baina ya ofisi hizi mbili ili kuisimamia Serikali" amesema Kichere.
Leo Novemba 3, 2019 Rais Magufuli, kupitia Katibu Mkuu kiongozi John Kijazi ametangaza kumteua Charles Kichere kuwa CAG mpya kuchukua nafasi ya Prof Mussa Assad ambaye muda wake unafika ukomo kesho Novemba 4, 2019.

No comments :
Post a Comment