Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 19, 2019

Hifadhi mpya ya mafuta yagunduliwa nchini Ghana!

Hifadhi ya mafuta yenye ujazo wa mapipa bilioni 1.2 imegunduliwa magharibi mwa nchi ya Ghana.

Taarifa iliyotolewa na shirika la utafiti na utengenezaji la Springfield (SEP) kupitia mkurugenzi wake Kevin Okyere ilisema kugunduliwa kwa mafuta magharibi mwa nchi hiyo ni tukio kubwa la kihistoria katika nchi hiyo.

Okyere, “Utafiti tuliouendesha katika mwambao wa bahari kwa kutumia meli ya utafutaji mafuta umetuwezesha kugundua mafuta ghafi ya ujazo  wa mapipa bilioni 1.2”.

Kazi hizo za kitafiti zilizofanywa katika maeneo 2 tofauti zilidumu takribani siku 40, Okyere aliongeza kwamba ugunduzi huo utakuwa ni hatua kubwa kwa shirika la kiafrika.

Ghana nchi ambayo katika historia inafahamika kama “ghuba ya dhahabu” mnamo mwaka 2016 dhahabu ilikuwa ni asilimia 42 yamauzo ya nje, Kuanzia mwaka 2010 Ghana ilianza kuvuna mafuta, ambayo pia yanachangia katika uchumi wa nchi hio.

No comments :

Post a Comment