Mtu mmoja ameuawa na wengine kujeruhiwa Jumamosi katika maandamano yaliyoshuhudiwa kote Iran, yanayopinga uamuzi wa serikali wa kusambaza mafuta ya petroli kwa mgao pamoja na kuyaongeza bei yake.
Shiriki la habari la serikali IRNA limesema maandamano yalikuwa makubwa zaidi jana usiku katika mji wa Sirjan.
Waandamanaji walivamia ghala ya mafuta na kujaribu kuichoma moto. Serikali ya Iran ambayo imekuwa ikipambana na vikwazi vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani, imetangaza kuongeza bei ya mafuta ya petroli Ijumaa kwa asimilia 50.
Inadai hatua hiyo inalenga kusaidia wananchi wanaohitaji msaada wa pesa.
Rais Hassan Rouhani ameahidi Jumamosi kwamba kwa sasa asilimia 75 ya wananchi wa Iran wanaishi maisha magumu, na mapato ya ziada yatakwenda kwao, na sio katika hazina ya serikali.

No comments :
Post a Comment