Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa mwito wa kufanyika uwekezaji zaidi barani Afrika ili kuboresha viwango vya hali ya maisha na kuzuia wahamiaji kukimbilia Ulaya, ikiwa ni sehemu ya mkakati ulioanzishwa na Ujerumani wakati ikishikilia urais wa mataifa yalioendelea kiviwanda na kuinukia kiuchumi duniani, G20.
Akikutana na viongozi kadhaa wa Afrika pamoja na taasisi washirika wa kibiashara wa kimataifa, Merkel amesema wanatakiwa kufanya kila juhudi kushirikiana na Afrika na sio kuzungumzia juu ya Afrika lakini kujaribu kufanya kitu cha pamoja na bara hilo.

Merkel amemkaribisha rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi pamoja na wakuu wengine wa mataifa ya Ethiopia, Benin, Ghana, Morocco, Tunisia na kwingineko katika mkutano wa mpango huo unaojulikana kama Compact with Afrika.
Amesema, kwa pamoja Afrika na Ulaya watanufaika na uwekezaji huo huku akisisitiza umuhimu wa uwazi zaidi barani Afrika, ili makampuni ya Ujerumani yawe na imani ya kutosha ya kuwekeza barani humo.
No comments :
Post a Comment