Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 18, 2019

Rais Dk. Shein aupongeza Umoja wa Kamati za Olympiki!


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepongeza uwamuzi wa Umoja wa Kamati za Olympiki kwa kuichagua Zanzibar kuwa mwenyeji wa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Kamati za Olympiki za Afrika (ANOCA).

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Kamati za Olympiki za Afrika Mustapha Berraf akiwa amefuatana na Ujumbe wake.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa uwamuzi wa Kamati hiyo ya Olympiki (ANOCA) kwa kushirikiana na Kamati ya Olympiki ya Tanzania (TOC) ni uwamuzi wa busara kwani unaendeleza mahusiano na mashirikiano mazuri yaliopo katika sekta ya michezo kwenye nchi za Bara la Afrika.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais huyo wa Umoja wa Kamati za Olympiki za Afrika Mustapha Berraf kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo na kueleza imani yake kwamba mafanikio zaidi yatapatikana katika Bara la Afrika kwenye sekta ya michezo.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza haja kwa Umoja huo kwa mashirikiano na Kamati ya Olympiki ya Tanzania ushirikiane na Wizara ya Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kutayarisha michezo ya Kimataifa na mashindano mengine hapa Zanzibar kwa lengo la kuimarisha sekta ya utalii, ajira kwa vijana, mashirikiano, amani pamoja na kujenga afya.

No comments :

Post a Comment