Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 20, 2019

Uchimbaji wa Madini ya Uranium kuwekewa kanuni za usalama ili kudhibiti madhara!


Wadau wa sekta mbalimbali wamekutana kujadili sheria,  kanuni zilizopo ili kuboresha  usalama wa mionzi hususan katika uchimbaji wa madini ya uranium  ili kuhakikisha usalama  wa watanzania kiwa ni pamoja na kuwawezesha watanzania kunufaika na madini hayo.

Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomic  Tanzani ,Profesa Lazaro Busagala amesema kuwa  taasisi mbalimbali zimekutana  ikiwemo Tume ya madini,Mwanasheria Mkuu wa serikali na Nemc lengo ni kuwa na sheria na kanuni inayomlinda Mtanzania na kuhakikisha madini yanayanufaisha Watanzania.


Mkaguzi Mkuu wa Migodi  na Mazingira kutoka Tume ya Madini ,Abdulrahman Mwanga amesema kuwa madini ya Uranium ni madini yanayoweza kutumika kama chanzo cha nushati pia kutumika kutengeneza silaha kali hivyo uwekaji wa kanuni na sheria utasaidia kudhibiti madini hayo ili yasilete madhara kwa watu na mazingira.

Kamishna Msaidizi wa madini nchini,Terence Ngole  amesema kuwa uchimbaji wa madini hayo bado haujaanza nchini kwani ulisimama kutokana na kushuka kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia ,kwa sasa wako kwenye mpango wa kuweka  kisheria ,kinanuni ili uchimbaji ukianza madhara yasijitokeze.

No comments :

Post a Comment