Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 29, 2019

Kiongozi CCM awapa ujumbe nzito kina mama!


NAIBU Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Dk Abdalah Juma Sadala alimaruf Mabodi amewashauri wakinamama visiwani humo kujikita zaidi katika kilimo cha asili ambacho kiwasaidia katika kuimarisha hali za afya na kuwainua kiuchumi katika familia zao.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mafunzo ya Kilimo hai kwa viongozi wa Umoja wa Wananwake Mkoa wa Mjini kichama ambapo mafunzo hayo yalikuwa yanalengo la kutanua wigo wa kiuchumi kwa wanawake ndani ya CCM.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mjini Asha Juma Abdallah na kufanyika Shakani Mkoa wa Mjini Unguja.

Naibu katibu Mkuu alisema kwamba wanawake wanapaswa kuchangamkia fursa iliyopo kwa kulima kilimo cha asili ambacho kitawasaidia katika kukuza hali zao za afya pamoja na kuimarisha afya zao.

Pia alisema Kilimo cha asili kitawasaidia kwa iasi kikubwa wakina mama hao katika kuwapatia mahitaji yao madogo madogo na kuzifanya familia kuwa imara zaidi.

“Wakulima wengi hususani wakina mama wameacha kulima kilimo ambacho cha asili kisichohitaji madawa wala makemicail ambapo tunaona kilimo hichi kinaida kubwa hasa katika kuwapatia afya njema pamoja na kuwainua hai zao za kiuchumi” alisema Dk Mabodi.

Dk Mabodi katika maelezo yake alieleza kwamba ikiwa kilimo kitatumika ipasavyo hakuna familia itkayo zalisha kijana au mtoto ambaye atakuwa ombaomba kutokana na kuwa kilimo ni kazi isikuwa na ubaguzi wa kijinsia ,dini,kabila wala rangi.

Alifahamisha kuwa kilimo kuwakilimo ni utu wa mgongo hivyo jamii hususani wakina mamawanapashwa kuwa mstari wa mbele katika kijikita na kilimo ambapo kimeonekana kina faida nyingi.

Hata hivyo aliwataka wahitimu wa mafunzo haya kuengeza thamani ya biashara zao ili kupata soko la uhakika ili lengo la mafunzo hayo yaweze kufikiwa.

Nae Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mjini Asha Juma abdallah alisema kwamba lengo la mafunzo hayo Kwa wakina mama hao ni kuwaonesha fursa yakijikwamua na umasikini lakini pia kuongeza wigo wa kipato kwao.

Aliongezakusema mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wakinamama hao namna ya kulima na kula vyakula ambavyo havita athiri afya zao.

Nao washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni UWT wamepongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa mjini kwa juhudi zake za kuanzisha chuo kinachotoa mafunzo yanayohusiana na kilimo cha mboga mboga ndani ya mkoa huo ,ambacho kitasaidia kujikomboa najanga la umasikini.

Mafunzo hayo yaliikuwa ya siku moja yaliendeshwa na Dk Matima Abdallah ambapo wanafunzi walisoma kwa nadharia na vitendo kupitia shamba darasa lililopo eneo la shkani.

No comments :

Post a Comment