Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 31, 2019

Mama Mzazi wa Mwanahabari Erick Kabendera afariki dunia!


Mama wa Mwanahabari Erick Kabendera amefariki dunia, familia imethibitisha. Bi Verdiana Mjwahuzi (81) amefikwa na umauti katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Alipelekwa hospitalini hapo siku ya Jumamosi wakati hali yake ikiwa mbaya. Hata hivyo kufikia mapema jana taarifa zilisema hali yake ilikuwa ikiendelea kuimarika.
Kabendera yupo rumande akikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi. Hivi karibuni mama Verdiana Mjwahuzi (81) alimuomba Rais John Magufuli kumsamehe mwanae.

Erick Kabendera alikamatwa mwezi Julai 2019 na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kuongoza kikundi cha uhalifu. Mashtaka ambayo mawakili wake wameyakana.

Tayari mawakili wake wamefungua majadiliano na mkurugenzi wa mashtaka wa serikali (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Wakati Kabendera anakamatwa, tayari afya ya mama yake ilikuwa dhoofu.


No comments :

Post a Comment