Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 25, 2019

Mpelelezi wa Umoja wa Mataifa afukua mazito mauaji ya Khashoggi!

Mpelelezi wa Umoja wa Mataifa, Agnes Callamard amesema hukumu ya kifo kwa watu watano nchini Saudi Arabia kutokana na mauaji ya mwandishi wa habari wa Kisaudia, Jamal Khashoggi, imesababisha hasira ulimwenguni kwa sababu wahusika halisi wa tukio hilo bado wapo huru.

Kwa mujibu wa Deutsche Welle imeripoti kuwa Bibi Callamard, mchunguzi maalum wa Umoja wa Mataifa aliyechunguza kifo cha Khashoggi, amesema atahakikisha kuwa hakuna mtu, bila kujali wadhifa au nguvu alizonazo, atakayeepuka kuwajibishwa iwapo alihusika na mauaji hayo.
Khashoggi, mwandishi wa habari aliyekuwa wakati mmoja karibu na familia ya kifalme ya Saudia, aliuawa na viungo vyake kukatwakatwa ndani ya ubalozi wa nchi yake mjini Istanbul, Uturuki, mwaka jana.

Siku ya Jumatatu, mahakama mjini Riyadh iliwahukumu watu watano kwa mauaji ya mwandishi huyo wa habari.

Mpelelezi wa Umoja wa Mataifa Agnes Callamard alipozungumza na shirika la habari la Ujerumani dpa ameyataja maamuzi katika kesi hiyo kuwa ni kejeli na kwamba anataka haki itendeke.

Callamard ametaka Saudi Arabia isipewe nafasi ya kuandaa mkutano wa kilele wa G 20 mwaka ujao.

No comments :

Post a Comment