Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Monday, December 30, 2019
Serikali ya Sudan na waasi wasaini mkataba wa amani!
Serikali ya Sudan na makundi tisa ya waasi Jumamosi wametia saini mkataba wa ratiba kuelekea kumaliza mgogoro wa umwagaji damu katika jimbo la Darfur.
Mkataba huo umeelezea masuala mbali mbali ambayo vyama vitahitajika kushauriana wakati wa duru ya mazungumzo mjini Juba.
Mpatanishi mkuu wa matatizo ya Darfur, Ahmed Mohamed kutoka Sudan Revolutionary Front-SRF ushirika wa makundi tisa ya waasi yaliyoshiriki kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan alisema wanaamini hii ni hatua moja muhimu.
Mohamed aliliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna shaka hatua hii itasaidia utaratibu wa kufanikisha amani ya kudumu huko Darfur na pia utafanikisha utaratibu wa serikali ya mpito huko Sudan kusonga mbele kwa utulivu bila kuwepo vizuizi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment