Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Wednesday, January 8, 2020
Barabara ya Koani - Jumbi Zanzibar yawekewa jiwe la msingi!
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuzijenga barabara kwa kiwango cha lami barabara ambazo hazijajengwa katika Mkoa wa Kusini ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na usumbufu.
Hayo ameyasema Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Salama Aboud Talib mara baada ya kuweka jiwe la msingi Barabara ya Koani Jumbi ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 56 Mapinduzi matukufu ya Januari 12.
Amesema katika kipindi cha miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar mtandao wa barabara za Unguja na Pemba umeimarika hivyo jitihada zitachukuliwa ili kuhakisha zinakuwa za kiwango kinachohitajika.
Aidha amesema kuimarika kwa miundo mbinu ya barabara ni moja ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya saba ya uongozi wa Dkt Ali Mohamed Shein.
Hata hivyo Waziri Salama aliwataka wakandarasi kuwa makini wanapojaza mikataba ya ujenzi wa barabara ili kuhakikisha ujenzi unamalizika kwa wakati ambao umepangwa.
Vilevile amewataka Madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara wawe wangalifu na kufuata alama ambazo zilizokwekwa ili kuondoa ajali zisizotarajiwa.
Pia amewata wananchi wa Zanzibar kuepuka kujenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuondosha usumbufu na kuepuka kuvunjia pale utanuzi unapohitajika kufanywa.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe amesema jitihda za kuimarisha miundo mbinu ya barabara zinaimarika kwa kuhakisha wananchi wa mjini na vijijini wananapata huduma zenye uhakika.
Aidha amesema katika kuhakisha wananchi wanajengewa barabara zenye ubora tayari Wizara imeweza kulipa fidia za vipando kwa wale wote waliongo’lewa.
Nae Mkandarasi wa Kampuni ya Mecco Nassor Ramadhan Korowa amesema watahakikisha ujenzi wa barabara ya Jumbi Koani unakamilika kwa wakati ili kuhakisha wananchi wanaondokana na usumbufu.
Ujenzi wa Barabara wa Jumbi Koani unatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 6.3 na upana wa mita 7 utagharimu Bilioni 5 na unatarajiwa kumaliza mwishoni mwa mwezi wa Febuari mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment