Ile Marekani tuliyokuwa tunaijua kuwa ni Super Power, imeipigishwa magoti na Jamhuri ya Kiislamu ya lran, baada ya kupata kipigo kikali asubuhi ya leo na kutangaza kuwa haina uwezo wa kuingia vitani na lran.
Huku ulimwengu ukiwa umesubiria jibu kali la Trump na maafisa wote wa Marekani, taarifa iliyotolewa na rais huyo wa Marekani (mcheza kamari) ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kwamba: (Mambo yako safi, tunafuatilia hasara iliyosababishwa na shambulio la lran kwenye kambi yetu kubwa ya kijeshi ya Ainil-Assad).
Hii ni katika hali ambayo kila mtu duniani alitarajia kusikia neno la Trump linalosema: 'Tutajibu.' Lakini imekuwa kinyume chake baada ya kubaini kuwa, lran sio taifa la kuchezea.
Lakini mbali na Trump, Waziri wa Ulinzi wa Marekani bwana Mark Esper amesema: "Tupo tayari kuhitimisha vita vya aina yoyote na lran." Akimaanisha kwamba hatuwezi kuingia vitani na Iran.
Lakini pia Lindsey Graham, Seneta wa chama cha Trump cha Republican naye ameandika: "Msijibu kabisa mashambulizi ya lran."
Aidha habari ndani ya lraq zimefichua kuwa, jeshi la Marekani katika kambi zilizoshambuliwa, limezuia waandishi wa habari kuonyesha hasara zilizotokana na kipigo cha leo cha lran na inasemekana linaficha miili ya askari wake walioangamizwa kama ambavyo linawasafirisha kisirisiri.
Aidha katika hali ya kushangaza jeshi hilo la kigaidi la Marekani limetangaza kwamba hakuna askari wake aliyeuawa, bali eti wale waliouawa ni raia wa lraq. Nayo serikali ya lraq imetangaza mapema leo kwamba, hakuna raia wake hata mmoja aliyeuawa wala kujeruhiwa katika kipigo hicho.
Aidha habari zinasema kwamba mamia ya askari wa Marekani wameonekana wakikimbia hovyo huku wengine wakiwa utupu, kwa kuwa shambulizi limefanyika majira ya saa saba za usiku wakiwa wamelala.
Aidha jeshi la lran limetangaza kwamba utitiri wa makombora yake kote nchini, yamewekwa tayari kwa ajili ya kushambulia maeneo yote ya kijeshi ya Marekani, iwapo Washington itajibu hata kidogo tu.
Hiki ni kipigo cha pili baada ya kile cha kutunguliwa ndege yake ya kisasa ya drone ya Global Howk ya Marekani miezi michache iliyopita.
Hii ndio lran na hii ndio Marekani. Kwa leo Iran imeithibitishia Marekani kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya lran ni Super Power.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment