Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 21, 2020

Rais Buhari 'amuangusha' Anthony Joshua!

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua alionekana akisujudu mbele ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mjini London.

Joshua ambaye ambaye ana mizizi yake nchini Nigeria pia aliambia umati uliokusanyika kwamba yuko tayari kusimama na Nigeria iwapo atahitajika.

Picha hizo zimetoa hisia tofauti katika mitandao ya kijamii , huku wakosoaji wa Buhari wakikasirika kwamba Joshua hakuzungumzia kuhusu changamoto zinazowakabilia vijana wa Nigeria.

Joshua alisema hivi katika chapisho lake la Instagram: Ni kuhusu utamaduni na heshima kwa viongozi wetu.


Wengine hatahivyo walimpongeza Joshua kwa kukumbatia mizizi yake ya Nigeria na kusujudu mbele ya rais Buhari - ikiwa ni hali ya kitamaduni kuonyesha heshima kwa wakubwa.

Rais BUhari yupo mjini London kwa mkutano wa uwekezaji ambao hufanyika kila mwaka tarehe 20 ya mwezi Januari. Picha za mkutano huo katika mji mkuu wa Uingereza pia zilichapishwa katika mtandao wa Youtube na kitengo cha habari nchini Nigeria.

No comments :

Post a Comment