Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 8, 2020

Shamsu vuai: Dhamira ya mapinduzi ya Zanzibar ni kumkomboa mwafrika!


WAZIRI Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha amesema Azma ya MapinduzI Matukufu ya Zanzibar ni kuwakomboa Waafrika na kuwajengea moyo wa kujiamini katika kutumikia Taifa.

Aliyasema haya leo huko katika ufunguaji wa majengo ya madarasa manne, Maabara mbili, Ukumbi wa mitihani na Ofisi za Walimu huko katika Skuli ya Sekondari ya Charawe ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Mapinduzi Matukufu kutimia miaka 56.
Alisema madarasa tulozindua ni dhahiri kuwa kuendeleza sekta ya elimu yanatekeleza Azma ya Mapinduzi Matukufu yakiwa na dhamira ya kulinda kwa vitendo ili kupata wataalamu bora.

Hivyo aliwaomba wanafunzi wasome kwa bidii kwani wakati waliposema wao kulikuwa hakuna madarasa kama ya leo wala maabara tofauti imezidi hivyo wathamini juhudi za Serikali katika kuzidisha mafanikio ya maendeleo kwa upande wa elimu.

“Tuzidi kumuunga mkono Rais wetu Dkt Shein kwa kujenga Skuli za Ghorofa zenye viwango na madarasa ya kisasa Unguja na Pemba Mjini na Vijijini”, alisema Shamsi.

Aidha Alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein kwa Utekelezaji wa ilani ya CCM katika kuendeleza yaliofanywa na Muasisi wa Mapinduzi matukufu yaliofanyika 1964.

Pia alisema maendeleo ya elimu yanazidi kuimarika na kupatikana mazingira yaliyo mazuri kwa kuwepo vifaa vyote vya maabara na mabuku pamoja na vitabu.

Hata hivyo Mheshimiwa Shamsi aliwaomba wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu na kamati za Skuli pamoja na masheha kuhakikisha kila mtoto aliyefikia muda wa kuandikishwa aandikishwe na kuanza masomo.

“Natoa wito kwa wazee wazazi na walimu pamoja na masheha kuwaandikisha watoto wote waliofikia umri wa kusoma wapelekwe skuli “,alisema mstaafu huyo.

Nae Naibu Waziri wa Elimuna Mafunzo ya Amali Simai Mohamed Said aliahidi kupitia Wizara kutatua changamoto zinazoikabili Skuli ya Charawe ikiwemo kupatiwa Kompyuta,pamoja na ukarabati wa skuli .

Aidha amesema watashughulikia posho la walimu wanaovuka kutoka Charawe kwenda Chwaka na kuongeza walimu ili wanafunzi wafaidike na matunda ya Mapinduzi kwa kujipatia elimu bure.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema changamoto zinazowakabili katika Mkoa huo ni wanafunzi kuwa wengi darasani na sasa wanasoma kwa wastani.

Vilevile alisema katika Skuli ya Mwera ipo changamoto ya kuwa watoto wengi kujaa darasani ila jitihada zaidi ya kuitatua changamoto hiyo ipo mbioni.

Mradi huo umegharimu Zaidi ya milioni mia moja ambapo pesa hizo zimetolewa na wananchi, viongozi wa majimbo na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

No comments :

Post a Comment