Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Wednesday, January 8, 2020
SMZ imesema itendelea kuwalinda na kuwatunza wazee!
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kwamba itaendelea kuwalinda, kuwatunza na kuwathamini wazee Nchini kutokana na kazi kubwa walioifanya katika arakati za kupigania uhuru wa Nchi sambamba na ujenzi wa Taifa.
Imesema hadi Nchi kufikia hapo juhudi kubwa zimefanywa na wazee ambapo kwa wakti wao ndio walioweza kuondosha utawala wa kidhalimu uliokuwa ukiwatala wazanzibar.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la makaazi ya wazee Sebleni ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra ya kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema Serekali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alijenga makaazi ya wazee ili na wao kuwa na furaha ya maisha baada ya kufanya kazi ngumu ya kuiletea maendeleo Zanzinbar.
“Wazee ni chachu ya kuleta maendeleo kwa Taifa lolote duniani kutokana na busara na hekima zao hivyo yafaa kutunzwa na kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuitumia hadhina waliyo nayo.’’ Alisema Waziri huyo.
Aidha alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekititi wa Baraza la Mapinduzi. Dkt Ali Muhamed Shein kwa kuendeleza yale yote yalioazishwa na Serekali ya awamu ya kwanza kwa kuimarisha Miondombinu iliyo bora, Afya na Elimu .
Na kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Uwezeshaji , Wazee ,Wanawake na Watoto. Fatma Gharib Bilali alisema lengo la Serikali kuendelea kukarabati majengo yaliyo chakaa ni kuhakikisha yanakarabatiwa na kuwa na haiba nzuri kama aliyo iwacha marehemu Mzee Abeid Amani Karume .
Zaidi ya shilingi milioni mia tatu ishirini zimetumika kukarabati jengo la makazi ya Wazee ambalo sehemu ya chini ya jengo hilo litatumika kwa shughuli za Kiofisi kwa Wizara ya Kazi , Uwezeshaji , Wazee , Wanawake na Watoto na sehemu ya juu itakuwa ni skuli itakayofundisha mafunzo ya Sheria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment