Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Wednesday, January 8, 2020
Waziri awataka wananchin kuacha tabia ya kujenga pembezoni mwa barabara.!
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar, Salama Aboud Talib amewataka wananchi kuacha tabia ya kujenga nyumba pembezoni mwa barabara ili kuepusha usumbufu kwa Serikali.
Amesema usumbufu ambao unaweza jitokeza pale ambapo Serikai itahitaji kufanya upanuzi wa barabara.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Koani – Jumbi yenye urefu wa kilimita 6.3, Hafla hiyo ni moja kati ya shamra shamra ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 56 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Salama Aboud Talib alisema kwamba Serikali huwa inaweka mikakati yake mbali mbali katika kuwafikia wananchi hudum mbali za kijamii hivyo ni busara kwao wananchi kujenga kwa kuzingatia mipango miji na kuacha kujenga pembezoni mwa barabara.
Alisema ni vyema kwa wananchi kufuata maelekezo ambayo wanapatiwa kabla ya kujnga ili kuepusha usumbufu ambao unaweza jitokeza pindi serikali itakapo hitaji kupanua miondombinu ya barabara.
“Rai yangu kwa wananchi kuepusha kujenga pembezoni mwa barabara ili kuepusha usumbufu kwa Serikali inapotaka kujenga au kupanua barabara” alieleza Waziri huyo.
Waziri huyo alieleza kwamba kukamilika kwa barabara hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli zao za kibiashara pamoja na kuepuka usumbufu wa usafiri jambo ambalo lilidumu kwa muda mrefu.
Aidha Waziri huyo alisema hakuna sababu za msingi zilizopelekea ucheleweshwaji wa ujezi wa barabara hiyo hivyo amemtaka mkandarasi aliyekabidhiwa barabara hiyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
“Hakuna sababu ya msingi ambayo tutaiopokea pindipo mkandarasi akichelewesha kukamilika kwa barabara hii, namuomba afanye kazi na kukamilisha kwa wakati” alisema Waziri huyo.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa barabara hiyo alisema kwamba ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilimita 6.3 unagharimu zaidi ya shilingi billion Tano za kitanzania.
Alifafanua kwamba kiasi ambacho kimeshalipwa ni zaidi ya Shilingi milioni 853 ikiwa sawa na asilimia 15 ya fedha zote.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed mahmoud alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo kutafungua hudama mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.
“Kukamilika kwa barabara hii itapelekea kuanzishwa na kufunguliwa kwa huduma nyingi za kijamii suala zima la Kilimo, biashara, afya pamoja na Elimu” alisema Mku huyo wa Mkoa.
Hata hivyo Mkuu huyo aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ inayoongozwa na Dk Shein kwa jitihada zakre mbali mbali za kuboresha miondombinu katika Mkoa huo wa Kusini Unguja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment