Kangi Lugola, Ni Bunge? HAPANA
By Zitto Kabwe, MP
Rais Magufuli anasema Kangi Lugola na wenzake wamesaini Mkataba bila ruhusa ya Bunge. Hii ndio standard? Mkataba Gani? Mbona kama hiyo ndio standard wengi hawapaswi kuwepo ofisini hata yeye mwenyewe.
Ujenzi wa Chato Airport Shs 69 bilioni haukupitishwa na BUNGE
Ununuzi wa Helkopta 13 USD 200m za kumlinda yeye Rais haukupitishwa na Bunge
Mkataba wa SGR haukupitishwa na Bunge, Shs 5 Trilioni
Mkataba wa passport mpya haukupitishwa na BUNGE, shs 230 bilioni
Ununuzi wa ndege haukupitishwa na BUNGE, 1.5 Trilioni. Juzi Serikali imesaini Mkataba na Boeing kununua ndege ya pili ya Dreamliner kwa Mkopo ( lease purchase) BILA RUHUSA YA BUNGE wala huo mkopo haumo kwenye mikopo iliyoruhusiwa na BUNGE.
Mkataba wa Barrick haukupitishwa na BUNGE
Rais aliidhinisha Fedha Shs 600 bilioni kutoka Benki Kuu ili kununua Korosho zilizoleta hasara ya USD 500m ( Shs 1.2 Trilioni) bila idhini ya Bunge.
Tangu lini Rais anaheshimu Bunge?
Kuna jambo. SIO HILI AMESEMA Rais. Najua kosa la Kangi kafanya Dili kwa kumzunguka Rais. Rais amekasirika. Rafiki yangu Kangi hakujua kuwa hakuna DILI nchini bila mkono wa Rais. Hoja ya BUNGE ni kisingizio tu.
Dar es Salaam
23/1/2020
No comments :
Post a Comment