dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 22, 2020

Serikali ya umoja wa kitaifa Sudan Kusini kuundwa leo!

Serikali ya umoja wa kitaifa inatarajiwa kuundwa leo nchini Sudan Kusini, baada ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kukubaliana kufanya hivyo siku ya Alhamisi.

Muda wa mwisho wa tatu uliowekwa kwa ajili ya kuunda serikali hiyo unakamilika leo. Hayo yanajiri baada ya Kiir kumteua Machar kuwa makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini.

Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei amesema sherehe za kuapishwa Machar na makamu wengine wa rais walioteuliwa zinafanyika leo.
Kiir na Machar walikubaliana katika mpango wa amani wa Septemba 2018 kuunda serikali hiyo, ingawa hatua hiyo ilicheleweshwa kutokana na kutokamilika kwa masuala muhimu kama vile idadi ya majimbo, kuundwa kwa jeshi la kitaifa na mipango ya ulinzi wa Machar ambaye amekuwa akiishi uhamishoni tangu mwaka 2016.

No comments :

Post a Comment