dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 12, 2020

CAG: SHEIKH PONDA ISSA PONDA AANZA KUPIGA CHAFYA!



UCHAMBUZI WA ACT KWA CAG. Leo 11.4.2020.

SHEIKH PONDA ISSA PONDA.

USHAURI.

Nimesoma kwa makini Uchambuzi wa Chama cha ACT Wazalendo leo Tarehe 11.4.2020.

Uchambuzi huo ni mzito sana kisiasa na kijamii. Hasa kwa Rais John Pombe Magufuli na Chama chake cha CCM.

Rai yangu naamini serikali inaowajibu mkubwa wa kukidhi kiu ya wananchi ya kutaka ukweli wa tuhuma nzito zilizoainishwa katika uchambuzi huo.
Na njia bora ni kufungua mijadala huru lakini muhimu zaidi kuchukua hatua za kisheria kwa wakosaji wa makosa ya kijinai kuwafikisha Mahakamani.

Katika hitimisho la uchambuzi wa ACT kuna fungu la maneno haya:

"Watanzania hatuwezi kuendelea kukamuliwa kila siku fedha huku zikifujwa na wachache wanaotulaghai eti ni wakombozi wetu. Wanatwambia: "Hapa Kazi tu" kumbe ni kazi ya kupiga hela za Watanzania".

Endapo mapendekezo ya kuwachukulia hatua wapigaji waliomo serikalini  wanaojificha nyuma ya matamko ya kisiasa ya hapa kazi tu maelezo na uchambuzi wa wataalam na wanasiasa kama ACT WAZALENDO walivyoonyesha kutakuwa na athari kubwa sana kwa Serikali na Chama chake cha CCM hasa katika mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu ujao.

SHEIKH
PONDA ISSA PONDA
0715536313

No comments :

Post a Comment