Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 9, 2020

COVID-19: SOAP - THE DEADLY CORONA VIRUS KILLER.!


JINSI SABUNI INAVYOANGAMIZA KIRUSI CHA CORONA NA KUKISAMBARATISHA KABISA.

Na: Mshinga JN

Ukimaliza kusoma share kuokoa maisha ya wengi.

Jina la ugonjwa: COVID-19
Jina la kirusi: SARS-Cov2

Kwa kifupi ugonjwa huu wa Corona ulipewa jina la COVID-19 huku kirusi kinachosababisha ugonjwa huu kikipewa jina la SARS-Cov2. Kwa hiyo tusichanganye tena haya majina mawili. 

kwa kiasi kikubwa jamii haijatilia maanani swala la kunawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara kama watalaamu wanavyotushauri.

Kwa nini sabuni na maji vimekuwa ni ngao muhimu sana kujikinga na ugonjwa wa COVID-19?

Je ni sabuni yoyote tu ama sabuni maalumu?

Je kipi bora zaidi kati ya sabuni na vitakasa mikono katika kuangamiza kirusi cha SARS-Cov2? 

Kabla ya kujibu maswali hayo nianze kwa kukielezea kirusi cha SARS-Cov2.

1. Kirusi cha SARS-Cov2 kinaingia mwilini kupitia sehemu tatu.

Machoni, puani na mdomoni.

Kirusi kikiwa bado nje ya mwili wa binadamu inawezekana kukiangamiza(kikiua: kwa lugha rahisi).

Kirusi kikishaingia ndani ya mwili hakuna dawa yoyote ya kukiangamiza ndio maana tunasema hakuna dawa ya kutibu huu ugonjwa.

2. Kirusi kinafikaje machoni, mdomoni na puani?

Kwa kiasi kikubwa kirusi kinafikia maeneo hayo matatu kiurahisi kabisa kwa kusafirishwa na viganja ama mikono yako mwenyewe kikitokea sehemu yoyote kilipoachwa na anayeugua COVID-19!

Kwa nadra kirusi hiki kinaweza kufika machoni, puani na mdomoni endapo mtu mwenye virusi amepiga chafya ama kukohoa mbele yako na kurusha majimaji ambayo yanatua usoni  kwako yakiwa na virusi tayari.

Njia nyingine ni through kissing ambayo inazuilika kirahisi.

3. Kirusi kinaweza kukaa sehemu yoyote hata kama imekauka kikisubiri mikono yako iguse tu kinate ili kipate usafiri wa kukipeleka puani, mdomoni ama machoni.

Kirusi kinaweza kuachwa na kukaa kwenye mbao, chuma, plastiki kwa masaa mengi ama hata siku kadhaa kikiwa na uwezo wa kuambukiza.

Na karibu kila kitu tunachoshika ama  kutumia ama  kimetengenezwa kwa plastic, chuma ama mbao.

4. Kwa lugha rahisi, Ngozi ya binadamu ni sumaku ya kirusi cha SARS-Cov2.

Yaani inauwezo wa kuvuta na kuvinatisha virusi kwenye ngozi yako ukishika tu vilipo.

Hivyo ukigusa tu kitu chochote ambacho kina virusi basi virusi hivyo vyote vinavyutwa na kuganda kwenye mkono wako.

Kumbuka mpaka hapa hujaambukizwa japo virusi vipo mkononi.

Utaambukizwa tu iwapo utanyayua mkono wako kushika macho, pua ama mdomo kwa sababu yoyote ile.

Hatari ni kwamba watu wengi hushika uso wao(Pua, mdomo ama macho) kila baada ya dakika 2,3,4 au 5. Ukishika tu tayari umejiambukiza mwenyewe.

Lakini pia tafiti zimeonesha ni vigumu sana mtu kutoshika uso wake kabisa. Ni kitendo anachofanya kila binadamu tangu utotoni.

Kitendo cha ngozi ya binadamu kuwa kama sumaku kwa kirusi hiki ndio sababu kubwa kabisa ya kwa nini kirusi  hiki kinasambaa na kuambukiza kwa kasi ya ajabu kuliko virusi vingine vyote ambavyo vimekuwepo  muda wote kama SARS-Cov, MERS nk.

5. Kirusi cha SARS-Cov2 kimeumbwa na mkusanyiko wa vimelea vitatu.

RNA, Protein na Lipids.

Hapa ndipo uchawi wote wa sabuni unapopatikana.

Ili tuelewane:

tukichukulie kirusi sawa na nyumba iliyojengwa kwa matofali.

Kwa ufananisho huo:

Protein ni sawa na matofali.

Lipids ni sawa na jointi zinazounganisha matofali(kifupi ni gundi ya kugandishia matofauli ili yashikane vizuri) na baadae lipids ni kama plasta ya nyumba kwa ukuta mzima.

RNA ni sawa na kitu chochote kinachohifadhiwa ndani ya nyumba. Hiki hatutakijadili hapa.

Kazi kubwa za lipids katika kirusi cha SARS-Cov2 ni tatu.

Moja: kuunganisha vimelea vya protein kujenga ukuta wa kirusi.

Pili: Kuweka ulinzi ili ukuta wa kirusi usiharibiwe. Sawa tu na kazi ya plasta kwenye nyumba.

Tatu: Lipids ndio inafanya mashambulizi ya kukiingiza kirusi ndani ya seli nyeupe mwilini baada ya mtu kuambukizwa na kupelekea mabalaa yote tunayoona.

Kwa hiyo ukiangamiza lipids basi kirusi kitaporomoka mithiri ya nyumba ya udongo inayoporomoka baada ya matofali kulowana na maji.

Tumalizie na sabuni sasa.

6. Sabuni yoyote bila kujali kama ni ya maji, ya mche ama ya kimiminika kizito ina kemikali ziitwazo kitaalamu  amphiphiles ambazo huwa zinafyonza ama kuyeyusha lipids yote ndani ya sekunde 20 tu. 

Hii ndio teknolojia inayotumika kuondoa uchafu kwenye nguo unapofua ama kwenye mwili unapooga.

Kwa sababu kirusi cha SARS-Cov2 kimejengwa na kupigwa plasta kwa kutumia lipids na sasa tunajua sabuni zote zinauwezo wa kufyonza hizo lipids ndani ya sekunde 20 tu. Hivyo,

Ukinawa maji na sabuni yoyote ndani ya sekunde 20 tu kirusi ambacho kipo mikononi mwako kinasambaratika chote muda huohuo mithiri ya nyumba inayoporomoka na kuanzia hapo ndio mwisho wa kirusi hicho.

Sabuni inayeshusha ama kufyonza lipids zote na kusababisha protein zote na RNA kusambaratika vipande vipande, na kuanzia hapo hicho si kirusi tena. Kwisha habari yake.

Hii ndio sababu ya kwa nini watalaamu wanashauri tupake sabuni na kusugua vizuri povu lake kwa angalau sekunde 20 ili kuruhusu kemikali za amphiphiles kukifikia kirusi na kufanya chemical reaction na kukiharibu kirusi kwa kukisambaratisha kabisa.

Hii ndio sababu tunashauriwa kunawa kwa maji na sabuni mara kwa mara kwa kuwa tunashika vitu vingi mara nyingi vinavyoweza kuwa na SARS-Cov2.

7. Kama hakuna sabuni na maji, inashauriwa kutumia sanitizer(vitakasa mikono). 

Lakini sabuni na maji lazima viwe chaguo la kwanza kabisa kwa kuwa ni bora kuliko sanitizer.

Vitakasa mikono vimetengenezwa kwa mchanyiko wa alcohol kama ethano ambayo nayo inauwezo wa kufyonza ama kuyeyusha lipids na kukisambaratisha kirusi endapo itakuwa na alcohol nyingi sana kati ya 60% mpaka 80%

Lakini watalaamu wanasema vitakasa mkono havina uwezo mkubwa na waajabu kama ule wa sabuni na maji ndio maana inashauriwa kwamba vitakasa mikono vitumike tu pale ambapo hakuna uwezano wa kupata maji na sabuni mfano ofisini, ukiwa ndani ya usafiri kama bus, treni, ndege nk. Ambako ni vigumu kuwa unawanawa mara kwa mara. 

Kwa hiyo kunawa kwa maji na sabuni mara kwa mara ni silaha namba moja ya kuzuia kupata ugonjwa wa COVID-19.

Vitakasa mikono vipakwe kila mara unaposhika kitu chochote kinachoweza kuwa na virusi lakini tu kama huna sabuni na maji. 

Vinginevyo nawa kwa sabuni na maji ndio komesha yake.

Sabuni na maji ni njia rahisi na isiyo ya gharama na wala hakuna haja ya kukimbilia hizo sabuni za gharama wanazopandisha bei baada ya kupata ufahamu huu wa kitaalamu.

Share zaidi kukoa wengine.

Na: Mshinga JN.

No comments :

Post a Comment