Mhe. Mbunge Ally Saleh akitoa mchango wake bungeni.
USHAURI KWA SMZ KUHUSU CORONA!
Sasa tuko miezi miwili tena ndani ya Corona na modeli tulochagua ni kutofunga bandarini, kutofanya lockdown ila tumechagua social distance, kukosha mikono na kuvaa barkoa.
Wakati hizo za kukaa masafa, kukosha mikono na barkoa zikiwa ndio silaha zetu za mstari wa mbele hali halisi sio ilivyo mitaani
Wito bado haujaitikiwa kwa maana ya kama watu tulio vitani. Suala la sehemu za ibada limeachwa kuwa la hiari kwa waumini wenyewe.
Wapo walofunga misikiti na pengine wapo walofunga makanisa. Na walio wazi tunatajia kuwa watachukua hatua za kinga.
Ofisi za Serikali zimeendelea kuwa wazi pamoja na baraza la wawakilishi, la muhimu ni kuchukua hatua za kujikinga.... Kukaa masafa, kunawa mikono na kuvaa barkoa
Sasa hoja yangu, lakini nimefunzwa kuwa ukiwa na maslahi katika jambo ueleze ili hoja yako ipimwe pamoja na uzito huo. Hili nitalolisema nina maslahi nalo japo nashauri kama mimi binafsi
Ushsuri wangu unatokana na maelezo ya uchambuzi hapo juu.
Yaani kama issue ni kufuata kinga za barkoa, kukaa masafa na kukosha mikono na kinga hizo zinafanywa Ofisi za Serikali, Baraza la Wawakilishi...Mabenki yakiendelea na kazi
Ni kwa nini vyuo visitengezewe protokali ili vifungiliwe baada ya ukaguzi mkamilifu wa wataalamu wa afya... Kwamba kila chuo kiweke miundo mbinu ya kunawia, miundo mbinu ya sanitizer points, kuwa na vipima joto kwa kuwapima wanafunzi kila siku, kuandaa utaratibu wa kukaa masafa na vyenginevyo kadri watavyoelekezwa
Almuradi vyuo vipewe masharti ya NEW NORMAL ili vifunguliwe
Nimesema vyuo kwa sababu ni watu wazima na wanaweza kujisinamia na kufuata masharti watayoelekezwa
Naamini hili tunaweza kuliamua kama Zanzibar na masharti yote ya kiafya kujali ugumu wa maradhi haya. Maana nimeanza kusikia milango ya utalii inaandakiwa kufunguliwa
Hoja yangu ni kuwa tunaanzaje kuishi na New Normal maana huu ugonjwa unaweza kuendelea kuwepo muda mrefu zaidi... Lazima tuanze maisha
Ally Saleh
Mbunge wa Malindi
No comments :
Post a Comment