dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 22, 2020

Nani ni nani Zanzibar 2020: Mfahamu Profesa Makame Mnyaa Mbarawa!

Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ni mmoja ya wanazuoni tajwa wa Zanzibar akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Uhandisi wa Baharini (Marine Engineering). Makala hii fupi inajikita kwenye kumfahamu kidogo Profesa Mbarawa, alipotoka, mchango wake kwa nchi yetu na nafasi yake katika historia yetu.

Chokocho, Unguja, Dar es Salaam, Urusi, Australia, Afrika Kusini, Dar es Salaam

Mbarawa alizaliwa kijiji cha Chokocho, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 12 Februari mwaka 1961, wakati huo Zanzibar ikiwa bado chini ya utawala wa Kisultani. Masomo yake ya awali, msingi na sekondari (hadi kidato cha tatu) alisoma huko huko Pemba na baadaye kutokana na uwezo wake mzuri wa kiakili darasani akapata nafasi kuendelea na masomo ya juu Unguja.


Mara tu baada ya uhuru, Zanzibar likiwa bado taifa changa lilianzisha mpango wa kuwapeleka masomoni ughaibuni vijana wake ili wapate ujuzi na kurudi kujenga nchi. Utaratibu huo uliendelea toka wakati huo huku wakinufaika Wazanzibari wengi na mwaka 1985 Mbarawa akiwa kijana wa miaka 24 naye akapata bahati ya kunufaika nao pale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ilipomtafutia nafasi na kumpa ufadhili kwenda masomoni nchini Urusi.

Mbarawa akaondoka Zanzibar kisha Dar es Salaam na baada ya safari ya siku kadhaa akawasili katika jiji la Astrakhan kusini mwa Urusi. Katika jiji hilo Mbarawa akawa mwanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Astrakhan (Astrakhan State Technical University). Alikaa hapo kwa miaka takribani 6 na kuhitimu akiwa na Shahada ya Uzamili (MSc) katika fani ya Uhandisi wa Mambo ya Bahari(Marine Engineering) mwaka 1992.

Astrakhan State Technical University Urusi alipofikia Mbarawa akitokea Zanzibar

Kitivo cha Teknolojia ya Bahari katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Astrakhan aliposoma Mbarawa

Mara baada ya kuhitimu, na kwa kufuata ushauri wa waalimu wake na viongozi wa SMZ wakati huo, ilionekana ni vyema Mbarawa akapata ufadhili mwingine toka serikalini na kumalizia kabisa kwa kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD). Uamuzi huo ulikusudia Mbarawa akimaliza arudi Zanzibar akiwa mtaalamu mbobezi kwenye uhandisi wa bahari ili afanye kazi na kulipa fadhili kwa walipa kodi masikini, wavuvi, wakulima na wafanyakazi wa Zanzibar. Baada ya ufadhili wake wa masomo hayo ya Uzamivu kuidhinishwa, Mbarawa akaelekea katika jiji la Sydney nchini Australia kwenye Chuo Kikuu cha New South Wales (UNSW) ambako alihitimu na kutunukiwa PhD yake mwaka 1999, akiwa na umri wa miaka 38.

Kama nilivyodokeza hapo awali, matarajio ya SMZ, wazazi, ndugu na watu wa karibu na Mbarawa yalikuwa kwamba baada ya masomo na utaalamu huo mkubwa alioupata Mbarawa angerudi Zanzibar na kushirikiana na serikali iliyompa fadhila ili kujenga nchi yake Zanzibar. Ndoto ilikuwa kwamba kijana huyu alosomeshwa kwa kodi za wananchi masikini wa Zanzibar angerudi kujiunga na SMZ kuwatumikia Wazanzibari lakini haikuwa hivyo.

Maisha ya Urusi na Australia kwa zaidi ya miaka 14 yakawa tayari yamembadili Mbarawa kimtazamo na fikra za kibepari, kibeberu na kimagharibi zikamtia upofu akaitosa Zanzibar na walipakodi wake masikini walomsomesha. Mbarawa hakurejea si tu kwenye ofisi za SMZ bali hata kwa wazee wake Chokocho na ardhi ya Zanzibar. Akabaki ughaibuni kutafuta malisho bora kwa kutumia elimu yake akisahau gharama ya kuipata ilikuwa ni jasho la kodi ya Wazanzibari. Hakuna rekodi yoyote SMZ wala Posta na PBZ kwamba Mbarawa aliwahi kutumia fedha alizopata katika ajira zake ughaibuni kulipa fedha ya walipakodi wa Zanzibar jambo ambalo lingekuwa afadhali kwani aliamua kuwatosa licha ya kugharamia elimu yake, kwa neno jingine usaliti kwa nchi yake na watu wake. Tunaposema usaliti, Mbarawa hakusaliti nchi peke bali alisaliti hata nduguze ambao inaelezwa hakuwahi kuwatumia fedha katika hali yao yoyote, hata pale wazazi wake walipougua na kuhitaji msaada toka kwa kijana wao.


Mfano wa fleti ambazo wanafunzi wenye kipato kiasi kutokana na kazi za ziada kama Mbarawa walikuwa wakiishi

Baadhi ya watu waliosoma naye Astrakhan Urusi wanasema kama SMZ ingeanza kumchunguza mapema ingegundua haraka kwamba Mbarawa aliitosa Zanzibar miezi michache tu baada ya kutua Urusi. Kwanza alijitenga sana na wanafunzi wenzake weusi alotoka nao Bara Afrika, pili katika kazi zake ndogo ndogo za kujiingizia kipato nje ya shule wakati wa mapumziko na majira ya baridi hakuwahi kuwasaidia wazazi wake walokuwa wakiishi kwenye nyumba duni yenye kuvuja paa Chokocho. Nani asojali wazazi wake mwenyewe anaweza kujali nchi na wananchi wake? Mbarawa yeye mapato yake ya ujanani akayatumia kwa starehe ambako rekodi zinaonesha pia alikuwa na mahusiano na wanawake wawili wa Urusi, mahusiano yaliyozaa watoto wawili mmoja sasa akiwa na umri wa miaka 31 na mwingine 29. Hawa hivi sasa wana urai wa Urusi baada ya Mbarawa kudaiwa kuwatelekeza. Wote wawili walizaliwa katika Hospitali ya FGBUZ Astrakhan Urusi, mama zao wakiwa raia wa Urusi. Nyingi ya taarifa hizi za maisha ya Mbarawa Urusi zinathibitishwa pia na wanafunzi wenzake toka Zanzibar alokuwa nao nchini Urusi.
Hospitali ya FGBUZ

Kutokana na usomi wake uliotokana na kujitoa kwa Wazanzibari masikini kumsaidia kwa kodi zao ili aweze kusoma, Mbarawa aliondoka Sydney Australia na kuhamia nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka 1999 baada ya kupata nafasi ya kazi nchini humo. Baada ya kufika Afrika Kusini aliajiriwa kama mtafiti katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch kwenye Jimbo la Western Cape. Kwa wanaoifahamu vyema Afrika Kusini katika jimbo hilo zaidi ya asilimia 75 ni Wazungu hivyo panafanana sana na Ulaya. Ni eneo la kimkakati kuishi kwa wasomi wengi wa Kiafrika waliosoma Ulaya na wanaotaka kufanya kazi Afrika lakini si kwa kurudi kwenye nchi zao. Inawafanya kujisikia yuko Ulaya (kutokana na mazingira na mshahara) huku akiwa Afrika.
Makazi ya Mbarawa na waalimu wenzake Chuo Kikuu cha Stellenbosch. Baadaye inaelezwa alirudi na kununua nyumba mwendo kiasi kutoka eneo hili.

Alidumu Chuo Kikuu cha Stellenbosch kwa mwaka mmoja na mwishoni mwa mwaka 2000 akahamia Pretoria hapo hapo Afrika Kusini kwenye Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Tshwane kama Mhadhiri katika kitivo cha Mechanical Engineering. Alifanya kazi hapo kwa miaka tisa akipanda ngazi hadi kuwa Profesa Msaidizi mwaka 2005 na baadaye Profesa kamili mwaka 2009. Katika muda wote huu (toka kuhamia Australia na baadaye Afrika Kusini) Mbarawa hakujali kwao licha ya kuombwa mara nyingi kurudi Zanzibar kusaidia maendeleo ya elimu na utafiti katika eneo lake la ubobezi (Uhandisi wa Bahari). Amenunua nyumba Pretoria Afrika Kusini ambayo bado anaimiliki.

Hulka yake

Wanaomfahamu toka Urusi wanasema ni mtu mwenye akili nzuri darasani na kujituma masomoni na vijana wanalo la kujifunza katika hilo lakini wanatoa onyo. Mbarawa ni mtu mbinafsi hasa kwa namna ambavyo aliisaliti Zanzibar na Wazanzibari masikini walomsomesha kwa kodi zao kupitia kilimo na uvuvi. Alijivika uzungu, ubeberu na umajinuni na kuisahau nchi yake akiamua kutumia jasho la kodi walovuja Wazanzibari masikini ili asome na yeye kwenda kutumikia nchi nyingine kwa maslahi yake binafsi. Inaelezwa kuwa akiwa Urusi na Australia kuna wakati alifikia hali ya hata kuukana Uzanzibari wake.

Kuingia katika siasa za Tanzania

Mwaka 2006 akiwa bado Profesa Msaidizi Chuo Kikuu cha Teknolojia Tshwane, Mbarawa alishawishiwa na aliyewahi kuwa Makamu wa Rais Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal kurejea nyumbani lakini bado aligoma hadi pale alipoahidiwa nafasi ya uongozi serikalini. Ahadi hiyo ikamvutia lakini akawa bado ana wasiwasi hivyo akaamua kutoacha kwanza kazi yake nchini Afrika Kusini mpaka mambo yawe na uhakika. Akaanza siasa akija Zanzibar mara moja moja na kurudi Afrika Kusini.Katika muda huu akajiunga na Chama Cha Mapinduzi na kusaidiwa kupata nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Akiwa katika nafasi hiyo akawa anakuja nchini kuhudhuria vikao kisha anarejea Afrika Kusini. Makada mbalimbali wa CCM hawakupendezwa na tabia hii ambayo ilionekana kutompa Mjumbe nafasi ya kufanya shughuli za chama na kuhusiana vyema na wananchama. Kioja kingine kilikuwa namna ambavyo alikuwa akizungumza Kiswahili kwani alikuwa kama kakisahau, wengi wenu mtakumbuka hili kwamba ilimbidi muda mwingi awe anachanganya Kiswahili na Kiingereza.
Tarehe 3 Julai 2015, Dk Bilal akiwa Makamu wa Rais na Profesa Mbarawa akiwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakiweka jiwe la msingi ofisi mpya ya TTCL Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba

Kwa miaka mitatu yani 2007 hadi mwanzoni mwa 2010 Mbarawa aligoma katu katu kurejea jumla jumla nchini akisema bado hana uhakika wa maisha yake kiuchumi iwapo atarejea jumla. Mwaka 2010 akashawishiwa kujaribu kugombea Ubunge katika jimbo la Mkanyageni kilipo kijiji cha chimbuko lake la Chokocho. Kutokana na watu wa kwao kuapa kwamba kwa usaliti wake dhidi ya wazazi wake na Zanzibar hawa takaa wamuunge mkono, Mbarawa akaanguka vibaya katika uchaguzi huo na kukosa hata kura za wana CCM.

Kosa hilo la kimaamuzi kwa CCM kumpitisha Mbarawa kugombea Ubunge Mkanyageni licha ya kwamba ilikuwa wazi kabisa kuwa hakubaliki lilisababisha pia kupungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kura za Urais katika jimbo hilo kwa mgombea wa CCM na kura hizo kwenda kwa mgombea wa upinzani kwani wengi walichukia kupelekwa jina la Mbarawa kugombania ubunge eneo ambalo ana dhambi ya kulisaliti na kwenda kutoa nguvu kazi yake kwa mabeberu, eneo ambalo hana wafuasi wala ushawishi licha kwamba ni kwao kwa kuzaliwa. Wenyewe wanamuita jina la “Roho Stoki Mpotevu”.

Baada ya kushindwa Ubunge Mkanyageni na kuipa madhila CCM kwenye jimbo hilo kwa upande wa kura za Urais Mbarawa akaingia katika msongo wa mawazo kwa wiki kadhaa ambako inaelezwa alirudi Afrika Kusini na kujifungia kwake mwezi mzima huku ugonjwa wake wa AUS (Alcohol Use Disorder) ukizidi. Ugonjwa huu kwa jina jengine ni tatizo la kunywa pombe mara nyingi kuliko inavyoshauriwa kiafya na kuitegemea pombe Kisaikolojia. Inaelezwa kuwa tabia ya kutia kilevi kupitiliza aliianza akiwa Urusi, mwaka 1991.

Mwishoni mwa 2010 Rais Kikwete akamteua kuwa Mbunge wakiwemo pia Bi Zakhia Hamdan Meghji na Shamsi Vua Nahodha. Mbarawa pia alipata nafasi ya Uwaziri chini ya utawala wa Rais Kikwete.

Kutokana na ujumbe alipata kwao Chokocho, Mkanyageni na Zanzibar kwa ujumla Mbarawa akawa na hofu kuthubutu tena kwenda kujaribu kugombea Ubunge na 2015 alipojaribu akafeli tena Jimbo likienda kwa CUF. Hivyo akaendelea kuishi kwa Ubunge wa kuteuliwa akitegemea sana uamuzi wa Rais aliye madarakani kupata teuzi hizo, kuanzia Kikwete hadi sasa Dk Magufuli.
Akijaribu tena kuomba Ubunge 2015 ambapo alianguka na Jimbo kuchukuliwa na Mgombea wa CUF



Tabia ya jumla kazini na mahusiano mengine binafsi

Yapo malalamiko mengi ya namna ambavyo amewaachisha watu kazi katika tasisi mbalimbali kikatili na kwa kutofuata taratibu wengi wakiwa hawana hatia bali kwa ugomvi binafsi. Katika elimu yake, nafasi zake na ajira zake hajawahi kusaidia lolote wazazi wake ambao wanaishi kwa kutegemea msaada wa wazee kutoka SMZ.

Hadi leo hajaomba msamaha baadhi ya wajumbe Mkanyageni ambao walipinga asipitishwe kugombea Ubunge kwa kutokuwa na sifa na kuwepo uwezekano wa kukidhalilisha chama. Inaelezwa aliwajibu vibaya na kuwatukana wajumbe hao kwamba wanafanya maamuzi kimasikini na kuwa sio lazima kupata kura zao kwani yeye msomi na madaraka kwake yatakuja tu.

Wazanzibari wanasubiri kwanza alipe fedha zilizotumika kumsomesha kisha yeye kutimkia Ulaya na Afrika Kusini baada ya kupata elimu badala ya kurudi Zanzibar kulipa jasho la walipakodi masikini. Alichofanya kwa Zanzibar ni sawa na kijiji kizima kikusanye kila kilicho nacho kikutume safari ya mbali kuleta dawa ya kutibu umasikini kisha wewe uende, upate dawa na kutokomea. Ni usaliti na laana hii inamtafuna Mbarawa kila akitaka kufanya siasa au kusema anaingia kwenye siasa kuhudumia Wazanzibari. Hawezi kuhudumia watu ambao hakuwahi kuwajali, na Wazanzibari wako macho, wanafahamu hilo.

Wachambuzi wa siasa za Zanzibar wanasema Mbarawa hana nafasi kwenye siasa za Zanzibar wala Tanzania. Hana ushawishi na ana historia nyeusi katika kuwajali kuanzia wazee wake hadi Wazanzibari. Anaonekana kama msaliti, mtu wa Kimagharibi ambaye kajiweka wazi mbele ya Wazanzibari kwamba si lolote kutokana na matendo yake toka akiwa kijana mdogo kwenye mambo yahusuyo maslahi ya Wazanzibari. Afanye toba na kuomba wazee wake msamaha na kurudisha kodi ya Wazanzibari iliyomsomesha na labda kwa hayo atasamehewa lakini si kupata nafasi ya uongozi wa umma hapa Zanzibar. Majuzi kagawa shilingi laki 300 kwa baadhi baadhi ya wajumbe wa NEC Zanzibar inasemekana kutafuta Urais 2020 akiungwa mkono na Waziri wa Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir (HOK) ambaye amekumbwa na kashfa mbalimbali miaka ya karibuni. Utumie fedha za maskini walipakodi wa Zanzibar kusoma Ulaya kisha ukimbilie ughaibuni miaka lukuki na kuwaacha solemba, urudi kwa kuahidiwa shibe ya tumbo lako, ukidhalilishe chama kwenye kura za Urais, utese watu kwa madaraka yako, utukane na kudharau wajumbe, Ubunge ushindwe, ujaribu Urais? Kioja.

Mwandishi wa makala hii amejitambulisha kwa majina ya Jaffar Mohamed Ame mkazi wa Chokocho, Pemba. Anapatikana kwa simu nambari 0777 420 034.



No comments :

Post a Comment