dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 13, 2020

Uchambuzi: Nafasi ya Profesa Makame Mbarawa kwenye Urais Zanzibar!


KWANZA BONYEZA LINK YA HAPA CHINI ILI USOME MAANDISHI YA JAFFAR MOHAMED AME MKAAZI WA CHOKOCHO, PEMBA, KUHUSU PROFESA MBARAWA!

https://zanzibarnikwetu.blogspot.com/2020/05/nani-ni-nani-zanzibar-2020-mfahamu.html

Mengi yamesemwa kuhusu nia ya Profesa Makame Mbarawa kugombea Urais Zanzibar 2020. Wapo waloandika makala zenye uwiano bora, wapo walomponda na kusema hana nafasi lakini pia wapo walomsifia. Makala hii inachambua pande mbili za mjadala na kumpa msomaji ama uwanja mpana wa kuwa na hitimisho lake mwenyewe au kuendelea na tafiti zaidi, kujaribu kuona ipi hasa nafasi ya Profesa Mbarawa katika mbio za Urais Zanzibar 2020.

Profesa Makame Mbarawa
Upande wa kwanza ni kutazama yale ambayo Profesa Mbarawa ameyabainisha kwa watu wake wa karibu kuwa sehemu ya vipaumbele vyake iwapo atafanikiwa kuwa Rais wa Zanzibar. Japo mara nyingi wagombea wa CCM hunadi ilani ya chama chao, sote twafahamu kwamba Rais anaweza kuamua kuchomekea na kutekeleza hata yale ambayo si ilani kwa asilimia mia moja alimradi tu yako katika maono yake.

Jambo la kwanza ni kuondoa ubadhirifu katika manunuzi ya umma. Moja ya eneo ambalo amelitaja mara nyingi katika viunga mbalimbali na watu wake wa karibu ni ununuzi kwa gharama kubwa wa meli mpya ya abiria ya MV Mapinduzi II ambayo watafiti wengi wanaonesha si mpya, haijaleta tija Zanzibar na ilinunuliwa kwa gharama isiyo sahihi ikigubikwa na rushwa na ufisadi.

Jambo la pili analotajwa kuwa na kiu nalo ni kuona SMZ inatengeneza mazingira ya watu kufanya biashara badala ya yenyewe kujaribu kufanya biashara. Kwenye hili anaelezwa kukerwa na madudu ya SMZ ya ununuzi wa gharama kubwa wa meli mbili za uvuvi, Sehewa 1 na Sehewa 2 ambazo SMZ haikulazimika kununua.
Mbarawa anasisitiza kuwa kazi ya SMZ si kuingia kwenye biashara bali kuweka mazingira mazuri ya kisera na sheria kwa sekta binafsi.

Kosa la tatu ambalo Mbarawa anatajwa kuahidi kulisahihisa ni lile la SMZ kuanzisha miradi mikubwa ambayo thamani yake imepita uhalisia na haijakamilika. Mifano ya miradi hiyo maarufu kama miradi zimwi na ya upigaji ni ujenzi wa jengo la abiria Uwanja wa Ndege Zanzibar, miradi ya maji, barabara zisizo na viwango Unguja na Pemba, miradi ya kuweka taa barabarani, mitaro ya maji na ile ya kamera za usalama (CCTV). Mbarawa anaamini miradi hii haikuwa na dira (vision) na usimamizi ipasavyo na imeiletea Zanzibar hasara kubwa.

Kosa la nne analotajwa kukusudia kurekebisha ni kuhakikisha hakuna tena matumizi yasio ya msingi ya fedha za ZSSF kujenga miradi mikubwa ambayo uchambuzi wake unaonesha ni hasara kubwa kwa serikali na pesa za wananchi. Mifano ya miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba za makaazi Mbweni na Kwahani, ujenzi wa viwanja vya burudani vya Kariakoo na Tibirinzi na ujenzi wa maduka ya kisasa Michenzani na Darajani.
Mbarawa anatajwa kuwa muumini wa kuijengea nguvu sekta binafsi na anasisitiza kwamba SMZ ilikosea kujiingiza katika miradi hiyo na badala yake ingeweza kutekelezwa moja kwa moja na sekta binafsi.

Jambo jengine linalotajwa katika mipango yake ya awali ni kupitia upya ubadhirifu mkubwa uliopelekea kupewa mwekezaji asie na uwezo kujenga Hoteli ya Bwawani.

Hoteli hiyo hivi sasa imekuwa magofu. Pia anatajwa kuweka bayana kwamba panapo majaliwa akapata ridhaa lazima kutazama sababu za kutokamilika ujenzi wa gati ya kisasa ya Mpigaduri.
Eneo la ujenzi wa gati ya kisasa ya Mpigaduri

Kabla ya hitimisho, tutazame upande wa pili wa mambo ambayo tunaweza kuyaita vikwazo. Hivi lazima Profesa Mbarawa kuviruka ili kufikia ndoto yake ya kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi wa Rais Zanzibar 2020.

Kikwazo cha kwanza kinatajwa ni kutokubalika vya kutosha Pemba ambako ni kwao. Tafiti zinaonyesha hata kabla ya zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kuzirudisha halijaanza tayari kuna dalili kwamba Profesa Mbarawa ameanza kuwa na wakati mgumu kupata wadhamini kwao Pemba. Ili aweze kufanikiwa ni lazima atengeneze mazingira kwanza ya kukubalika na watu wa kwao.

Pili, inasemekana kwamba Profesa Mbarawa hajakwenda kumuona Rais wa Zanzibar Dk Shein muda mrefu. Hii inaleta ukakasi katika kuungwa kwake mkono. Katika siasa Rais aliye madarakani hasa kama anatoka chama chako ni mtu mwenye nguvu sana kwenye hatma yako. Kwakuwa muda bado kiasi tutegemee kumuona Profesa Mbarawa akijaribu kusahihisha hili kwa kwenda kumuona Rais na kwa namna fulani kuomba kuungwa mkono.

Jambo la tatu ambalo lazima kiunzi chake akiruke ni tuhuma za kuwa na mke Rai wa Uganda. Wazanzibari na hakika Watanzania ni watu wanaokumbatia sana utaifa na japo wanaweza kujinadi kwamba wanaheshimu na kujali watu wote, ni watu tofauti sana wanapoona mtu anayetaka ridhaa ya kuwaongoza ana mke mgeni. Bado ni ngumu kufahamu mbinu gani itatumika kupindua mjadala wa jambo hilo lakini ni jambo ambalo huenda likawa na mjadala mkubwa katika maamuzi ya CCM kwani lina athari kwenye sanduku la kura.

Taarifa za ugomvi wake na Bi Saada Mkuya nazo huenda zikaibuka na lazima kupatiwa maelezo. Inaelezwa kwamba katika utawala wa awamu ya nne Mbarawa akiwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia aligombana na Bi Saada kutokana na kile kilochotajwa Mbarawa kutoijali Zanzibar na kwa kuipa kipaumbele kwenye miradi. Hii inaweza kutumika kama taarifa ya kuhoji mapenzi yake kwa Zanzibar na huenda ikamtesa katika uchaguzi.

Jambo jengine linaloweza kuwa kiunzi kwake na lazima kutafutiwa maelezo mapema ni kiwango cha mali zake ambazo kazipata katika kipindi kifupi cha utumishi wake serikalini. Mali mbalimbali zimeanza kutajwa kama shamba kubwa la mikarafuu analomiliki Pemba, nyumba ya ghorofa Mbweni jijini Dar es Salaam na kadhalika.

Viunzi hivyo vyaweza kuchukuliwa kama vita ya kisiasa ya wapinzani wake kuibua mapungufu yake lakini ni mambo muhimu ambayo lazima ajiandae vyema kuyaondoa njiani. Iwapo atafanikiwa na malengo yake juu ya Zanzibar yakaeleweka na wengi basi anaweza kuwa na nuru kwenye nia yake, kinyume na hapo nafasi yake kwenye mbio za Urais 2020 itazidi kudidimia.



1 comment :

  1. Attention please !I am urgently in need of Kidney donors with the sum of $500,000.00,WHATSAP: +91 91082 56518
    Email: ( jainhospitalcare@gmail.com ) Thank you
    Please Share !

    ReplyDelete