Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kupokea maoni ya Vyama yya Siasa na Wananchi kwa ujumla kuhusu kupitia upya mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi Zanzibar. Sisi ACT Wazaendo tunaweka wazi msimamo wetu hatuungi mkono zoezi la ukataji upya wa Majimbo kwani ni kinyume na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inayotaka ukataji wa Majimbo ufanyike kati ya miaka 8 hadi 10. ZEC ilikata Majimbo mwaka 2015 tunajiuliza kipi kimeipelekea ZEC baada ya miaka 5 tu inakata upya Majimbo ya Uchaguzi? Pia katika kukata Majimbo kuna vigezo vilivyowekwa kikatiba kama ndio muongozo wa ukataji Majimbo, ikiwa ni pamoja na mipaka ya kiutawala, njia za usafiri, idadi ya watu na uwakilishi kati ya wananchi wa mjini na vijijini. Vigezo hivi hukiukwa na ZEC kwa makusudi ili kuinufaisha CCM.
Wakati ZEC wakijidanganya wenyewe kwa kudhani wanawadanganya Wazanzibari na dunia kwaujumla, kwa kutuaminisha kuwa wanakusanya maoni ya Wadau wa Uchaguzi ili wayatumie maoni hayo kama msingi katika ukataji wa Majimbo. Kuna taarifa za kuaminika kuwa ZEC na CCM wameshafanya maamuzi ya namna ya ukataji Majimbo kwa kupunguza Majimbo, kutoka Majimbo 54 hadi Majimbo 50. Upunguzaji huu wa Majimbo utafanyika kwa kupunguza Majimbo 2 Pemba, hivyo Pemba itabaki na Majimbo 16 badala ya Majimbo 18 ya sasa na Majimbo mengine 2 yatapunguzwa kutoka Wilaya za Magharibi A na B.
ACT Wazalendo haishangazwi hata kidogo na hilo. Kwetu sisi ni ithibati ya namna ZEC na CCM wanavyotapatapa katika kubebana wakati ubeleko umeshakatika. Kila ZEC Wanapopitia upya mipaka ya Majimbo na kukata upya Majimbo, dhamira yao ni kuibeba CCM na matokeo yake ni hujikuta CCM ikiwa haisaidiliki kwa lolote.
Mwaka 2015, ZEC ilipokata upya Majimbo haikuisadia CCM kwa chochote na ukataji huu pia hautoisaidia CCM kwa lolote. Tunachojivunia ACT Wazaalendo ni mtaji wa kuungwa mkono na Umma. Umma ndio mtaji wa ushindi wa Uchaguzi wowote.
Masikitko yetu ni kuona namna CCM na Serikali yake inavyoendeleza ubaguzi kwa Wananchi wa Pemba kwa kudharau Uwakilishi wa Wapemba katika vyombo vya maamuzi. Tunayasema haya kwani suala la kujiuliza, Vipi leo Pemba ambayo haikoongezewa hata jimbo 1 wakati ZEC ilipokata Majimbo upya mwaka 2015 leo ipunguziwe Majimbo 2 kama sio chuki na ubaguzi dhidi ya Wapemba. Pemba iliyokuwa na Majimbo 21 katika ya Majimbo 50, Mwaka 2000, yakapunguzwa kuwa Majimbo 18 tu na sasa ZEC na CCM wanataka Pemba iwe na Majimbo 16 tu.
ACT Wazalendo inawakumbusha CCM na ZEC kuwa mwaka 2015 ilipokata Majimbo Wananchi wa Zanzibar waliyapokea kwa shangwe na kuyapa msemo kuwa ni mkato wa kashata, vyovyote itakavyokatwa utamu wake ni ule ule. Hivyo na kwa hili linalopangwa na ZEC na CCM tunalisubiri kwa hamu litokee. Wazanzibari wako tayari kwa mabadiliko kukamilisha kazi waliyoifanya mwaka 2015.
Nassor Ahmed Mazrui
Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Mei 30, 2020

No comments :
Post a Comment