dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 20, 2020

DR. SHEIN AFANYA UTEUZI ZANZIBAR!

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya jana tarehe 19 Juni 2020, uteuzi wa wenyeviti wa Bodi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Dkt. Fadhila Hemed Ali ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Zanzibar.

2. Dkt. Ali Makame Ussi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi, Zanzibar.

3. Profesa Saleh Idriss Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo, Zanzibar.
4. Bwana Mohamed Suleiman Zidi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Barabara, Zanzibar.

5. Bwana Mtoro Almasi Ali ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani, Zanzibar.

6. Bwana Muhsin Muhammad Ali ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Karakana Kuu ya Serikali.

7. Bwana Kassim Maalim Suleiman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba, Zanzibar.

8. Bwana Khalifa Hassan Chum ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ujenzi ya Serikali.

9. Dkt. Mzee Suleiman Mdewa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Serikali Mtandao, Zanzibar.

10. Dkt. Abdulla Ismail Kanduru ameteulwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Elimu, Zanzibar.

11. Dkt. Salum Seif Salum ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wataalam wa Maabara za Masuala ya Afya.

12. Dkt. Ahmada Hamad Khatib ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo, Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza jana tarehe 19 Juni 2020.

No comments :

Post a Comment