Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Duu!!! Huyu kaka anasema kweli. Ile bei iliotangazwa ni face value tu. Hata mtu angelikuwa na kilo moja moja mpaka ikafikia idadi ile basi angelilipwa kwa bei ie ile. Bei ya uniqueness anayoisema kaka Lema haikutiwa kabisa. Kwa hapa nchi imepoteza. Inabidi tukubali kuwa tumekurupuka wakati tungeliweka bei yoyote tunayoitaka na Tanzanite ikazidi umaarufu na ikawa yenye thamani zaidi kuliko thamani tuliyoiweka. Sasa wakubwa watatuwekea wao bei na thamani ya Tanzanite, ksababu wenyewe tumeshindwa. Lini tena tutapata uzito kama ule wa Tanzanite? Tumeipoteza bahati yetu kwa siasa nyingi. Jamani nchi tuiendeshe kwa pamoja. Kidole kimoja hakivunji chawa. Hakuna mpinzani hapa, sote tunaitakia kheri nchi yetu. Hatuna nchi nyengine kama sio hii.
ReplyDelete