dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 21, 2020

MJUE MHE. MRISHO GAMBO!


MRISHO GAMBO

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Alizaliwa Mei 22, mwaka 1982 katika Hospitali ya Ocean Road ya Dar es Salaam.

Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ilala Boma na kuhitimu darasa la saba mwaka 1997 na kupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, katika Shule ya Sekondari Kibaha na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2001.

Mwaka 2002 alichaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Ufundi Tanga, maarufu kama Tanga Technical School. Alihitimu kidato cha sita mwaka 2004.


Mwaka 2005 alichaguliwa kujiunga na elimu ya juu, katika Chuo cha Uhasibu Arusha, kusomea stashahada ya juu katika Sayansi ya Kompyuta (Computer Science) na kuhitimu mwaka 2008.

Mwaka 2009 aliajiriwa kwa nafasi ya Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Mwaka 2011, aliajiriwa kama Msimamizi Mwandamizi wa Mifumo ya Kompyuta wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Nelson Mandela.

Mwaka 2011 alijiuzulu nafasi hiyo pale Chuo cha Nelson Mandela na kurudi Jiji la Arusha. Aliweza kurudi Jiji la Arusha kwa kuwa hakuwa ameacha kazi, bali aliomba likizo bila malipo.

Mwaka 2010 alijiunga tena Chuo cha Uhasibu Arusha kusoma Shahada ya Uzamili (Masters Degree) katika masuala ya Uongozi na Teknolojia ya Habari (Master of Business Administration and Information Technology) and na kuhitimu mwaka 2011.

April 2012 aligombea ubunge wa Afrika Mashariki na kushika nafasi ya sita kati ya watu 81 waliogombea.

May 2012 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

Julai 2016 aliapa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Agosti 18, 2016 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Felix Kijiko Ntibenda.




No comments :

Post a Comment