Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Wednesday, June 3, 2020
PDS YA ZANZIBAR YAANDIKA ........
"Assalaamu alaikum.
Alhamdu lillah, Tayari tumeshakamilisha madarasa 2 ambayo yapo tayari kabisa kuanza kazi mara baada ya Corona Virus Inshaallah.
Tunatoa Shukran kwa wote walio-donate ktk kufikisha jengo hili hapa lilipofika.
Natamani na lile darasa la Toronto pia tulimalizie hadi finishing kama hivi.
Naomba nikumbushie kuwa Watu wa Toronto wako na mtoto huku PDS anahitaji kuendelezwa.
Mtoto wenyewe ni hili Toronto class room ambalo limeambatana na ofisi.
Pia tunatoa fursa kwa organization ama individuals ambao wanataka ku-support wanafunzi ambao ni mayatima na ambao wana special talents.
Tutachukua wanafunzi 60 ambao wote hali zao za maisha ni duni.
Sasa tunakusudia kuwapa uniform, mabuku, vitabu, viatu, begi na hata penseli na mistari for free.
Vyote hivyo vitagharimu dola 20 za US.
Sasa unaweza ku-support mtoto mmoja, wawili au kwa mujibu wa uwezo wako
Kila mtoto mmoja anahitaji dola 20 kupata vitu vyote vilivyotajwa hapo juu
(Angalia picha za jengo la skuli ya PDS hapa chini)
Thank u
Together we can".
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment