dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 5, 2020

PEMBA: AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL NEEDS YOUR HELP!

Skuli ya kiislamu ☝☝ Ambasha Islamic high school Pemba, Ni skuli ya jamii iliyojengwa kwa kujitoleya. Skuli ipo maeneo ya shengejuu wilaya ya Wete. Skuli Ni boarding.

Msingi wa mafunzo Yao Ni maadili na silka za kizanzibari. Na imejizolea heshima na sifa kubwa kwa malezi mema na jitihada kubwa katika ufundishaji. Kuna wazanzibari wako daresalaam, lakini wameamua kuleta watoto wait Ambasha kuja kusomeshwa elimu na malezi ya kizanzibari.

Skuli imeanza form 1 Hadi form 4 katika fani za sayansi, biashara na art. Mwaka Jana 2019, form 4 ya mwanzo ilihitimu vizuri ikiwa na wanafunzi 31 waliohitimu katika division 1, 2 na 3. Hakukua na division 4 na zero hata mmoja.


Katika mafanikio hayo, uongozi wa skuli umeamua sasa kuanzisha masomo ya form 5 na form 6.

Ili kufikia lengo hili, ilibidi pajengwe madarasa ya maabara na madarasa ya kusomea. Majengo ya maabara yamekamilika, liliobaki Ni madarasa ya kusomea.

Kwa kutumia michango na ujenzi wa kujitolea, tayari madarasa matano yamejengwa na kufikia hatua ya kuezeka, ambapo bati 300 zinahitajika.

Mchango wako wa bati moja,mbili tatu au idadi yoyote unahitajika Sana.

Mayahudi wengi walioko ulaya na marekani fakhari Yao Ni kujitahidi kuwarudisha watoto nchini Israel kuja kusomeshwa elimu ya dunia na silka na utamaduni wa kiyahudi.

Ni muhimu Sana tuisaidie skuli ya kiislamu ya Ambasha itimize malengo yake.

Unaweza kuwasiliana na:

 Shk SALIM JUMA HAROUN 0777432331 

ili aje mwenyewe ama na gari ya keri au kanta kuchukua mchango wako wa bati.

Wabillahi Taufiik

No comments :

Post a Comment