zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 30, 2020

THE HUNTER HON. ALLY SALEH NOW BECOMES THE HUNTED - A CHANGE OF ROLES IN A POLITICAL GAME OF HUNTING!

Above: The maverick and the flamboyant Hon. Ally Saleh who is being criticized for doing nothing for his Malindi Constituency in the last 5 years except white-washing the walls of one dilapidated school.

"Assalam alaykum.
Naomba
nianze kwa kusema, Mimi si mwandishi mzuri sana kama Mbunge wangu alivyobobea katika fani ya Uandishi, lakini kubwa nililoliona katika waraka wa Ally Saleh ni kutawala kwa maandishi ya Uongo, miongoni mwa mambo alioyaeleza mbunge kuwa ametufanyia wana wa Malindi ni pamoja na kujenga skuli!! najiuliza Kuna skuli gani iliyojengwa katika Jimbo la Malindi ndani ya kipindi cha miaka mitano hii inayomalizika!? au Huko kupaka Chokaa kuta za skuli iliyochoka yenye Ubovu wa madirisha mpaka kufikia kuhatarisha maisha ya watoto wetu ukizingatia Skuli hizo ni za ghorofa ndio ujenzi wenyewe huo!



Kama anavyosema mwenyewe Ndugu ally Saleh kuwa, kazi ya mbunge sio kusaidia watu bali ni kuisimamia Serikali, basi ingekuwa ni jambo la busara sanna angeisimamia Serikali na kuhakikisha Madirisha ya Skuli ya Kajificheni na yale ya Skuli ya Darajani yanatengenezwa ili kunusuru Uhai wa watoto wetu, leo hii ukipita kajificheni utakuta madirisha yaliopo katika ghorofa yanavyohatarisha usalama wa watoto wetu, hili lingekuwa jambo jema zaid kuliko kule kuipaka Chokaa skuli hio kisha kujitapa kuwa Umetekeleza Ujenzi wa Skuli ya Kajificheni!!

Mbunge Ally angekuwa hajui maana ya ujenzi ni nini, ningeweza kumkubalia, lakini nafahamu uzuri anafahamu maana ya ujenzi, kwani anafanya ujenzi kabambe wa hoteli ya kitalii kule Chwaka. Mbona kule hapaki chokaa tu?

Eti Ally ajenge Skuli! Salaalee, hivi ikiwa ujenzi wa hozi tu alioombwa na na vijana wanaokosha magari pale Kinazini ni miaka mitano imeshapita hajawatekelezea unadhani ataweza lipi tena!? Vijana wa kinazini walikuwa ngome imara ya wapinzani wetu (CCM) Watu wakafanya kazi, vijana wakaelimishwa, hatimae wakajiunga nasi katika ukombozi. Badala ya kuwatia moyo, kuwapa faraja na kuwaonesha huku kuzuri, Mbunge ameshindwa hata kufanya harambee ili wapate Hozi la Maji. Leo mtu huyu ajenge skuli, tena skuli yenyewe ya serikali, kama si uongo ni nini?

Ukweli ni kwamba Ally Saleh alishatuwacha na kutusahau kimahitaji wapiga kura wake wa Jimbo la Malindi ambao tangu tumchague hajawahipo hatta kutukusanya wana Jimbo alau kwa kutwambia neno dogo tu la kiungwana "AHSANTENI"

By; mpiga kura wako h.k.a"

No comments :

Post a Comment