Yussuf Ali Juma (kushoto) na Mberwa Hamad Mberwa (kulia)
Mbarawa ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitajwa kuhusudu nafasi hiyo ameanza kampeni zake za ndani ya CCM akitafutwa kuungwa mkono na wajumbe wa chama hicho. Hapo jana akiwa Mkoani Pemba amefanya kikao na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma na mwenzake wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa.
Haijawekwa wazi mazungumzo yao yalihusu jambo gani hasa katika uchaguzi huo. Awali CCM ilitangaza zoezi la kuchukua fomu kwa watia nia lingeanza Juni 2 lakini baadaye muda huo ukasogezwa mbele hadi pale Bunge likatapovunjwa.
Profesa Mbarawa anadaiwa kuungwa mkono na Wabara huku wahafidhina wa Zanzibar wakisemekana kumtaka Meja Jenerali mstaafu Issa Suleiman Nassor (Taulo). Kanuni za CCM zinaonyesha kwamba Wanec ndio wenye nguvu ya kuchagua mgombea kupitia vikao na kura, na kama ni kweli Mbarawa keshapita kwa kuwa ni chaguo la Wabara kwa Zanzibar kama inavyodaiwa basi Wanec watakwenda Dodoma kutalii tu bila kazi yoyote ya msingi.
No comments :
Post a Comment