Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 2, 2020

ZAIDI YA WANANCHI 1200 WA JIMBO LA OLE WANYIMWA VITAMBULISHO VYA UZANZIBAR UKAAZI!

ZAIDI ya Wananchi 1200 wa Jimbo la Ole Mkoa wa Kusini Pemba wamenyimwa haki yao ya vitambulisho vya Uzanzibari ukaazi.

Jimbo la Ole ambalo ni miongoni mwa Majimbo ya Mkoa wa Kusini Pemba yanayoendelea na Zoezi la Uandikishaji pamoja na UHAKIKI wa taarifa za wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, huku zoezi hilo linaloendelea likiwa limeacha makovu makubwa kwa wananchi wa Jimbo la Ole na Pemba kwa ujumla.
Asilimia 99 ya wananchi hawa wanavyo Vitambulisho vyao vya Uzanzibari ambavyo bado havijamaliza muda wake, wanavyo Vitambulisho walivyotumia Kupigia Kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na wananchi wote hao wanazo risiti ambazo zimekusanya taarifa sahihi za mwananchi katika eneo husika, Suala hapa ni kwa nini kama kuna nia njema Wananchi hawa wasiandikishwe katika Daftari la kupigia Kura kwa kutumia taarifa hizo?

Kitambulisho cha Uzanzibari Ukaazi kwa Mzanzibari na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni haki ya kila mwananchi mwenye sifa zilizoainishwa kuweza kupatiwa, Makao Makuu ya ofisi ya Wakala wa Matukio ya Kijamii ambayo ndio taasisi inayohusika na kutoa Vitambulisho hivyo wamekiri kwamba Vitambulisho vimekamilika na vimefikishwa katika mawilaya husika kwa ajili ya Wananchi kuchukua, lakini kwanini Wananchi wanasumbuliwa na kuambiwa Vitambulisho havipo?

Ili Mwananchi apate fursa ya kuingia katika daftari la orodha ya Wapiga Kura, sheria inamlazimu awe na Kitambulisho hicho cha Uzanzibari Ukaazi, na kwa mujibu wa Ratiba ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Tarehe 1 na 2 mwezi huu wa June uandikishaji utafanyika katika Mkoa wa Kusini Pemba ambapo Jimbo la Ole lipo ndani yake. Siku moja imeisha ilhali zaidi ya wananchi 1200 hawajui khatma yao.

Je wananchi hawa sio Wazanzibar, Wananchi hawa hawana haki yakumiliki Kitambulisho cha Uzanzibar Ukaazi, Wananchi hawa hawana haki ya kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na kushiriki mchakato wa Kidemokrasia wa kuchagua Viongozi wanaowataka kwa muda wa miaka mitano (5) ijayo?, Ni nani atakae yasemea mahitaji na Changamoto za wananchi hawa ikiwa mutawanyima fursa ya kuchagua kiongozi wanaemtaka na wanaemuamini kuwakilisha na kutetea maslahi yao?

Kwanini Watawala wanaojinasibu kufanya vizuri wanakuwa waoga kwa wananchi ambao mumewatawala kwa zaidi ya miaka 50?

Tunatoa wito kwa Mamlaka husika kutekeleza wajibu wao kwa Uadilifu na Haki. Aidha tunawataka Wananchi wa Pemba kuendelea kudai haki zao za Kikatiba bila kuchoka wala kukubali kukatishwa tamaa.


Abeid Khamis Bakar
Katibu Idara ya Habari na Uenezi
Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa.


No comments :

Post a Comment