Membe ambaye hivi karibuni alitimuliwa CCM kwa kukiuka taratibu za chama hicho amesema kabla hajafikiria kujiunga na chama hicho alisoma katiba yao na kuielewa na kwa maono yake amesema ACT ndicho chama pekee cha upinzani kinachokua kwa kasi hapa nchini.
“Kwa hiari yangu nimeamua kujiunga katika familia kubwa ya ACT Wazalendo inayotaka mabadiliko yenye lengo la kuwanufaisha Watanzania wengi hasa wakulima, wafanyabiashara, watumishi wa serikali, wafanyakazi mbalimbali na wote wanaoitakia kheri Tanzania yetu. Nataka kupigania mabadiliko ya kweli ya hii nchi kupitia ACT na azma yangu itatimia.
“Sijawahi kuona kijana asiye na tamaa kama Zitto Kabwe, unaweza ukafika wakati wa uchaguzi akasema hagombei, huyu hana tamaa lakini hatma ya nchi hii iko mikononi mwake; huyu ndiye jasiri kiongozi, usipoteze ujasiri ulionao sisi tuko hapa kukusaidia.
“Maalim Seif amenilea tangu mwaka 1984 nyie hamumjui sijawahi kuona mwana– CCM aliyeyevumilia yasiyovumilika kama huyu, CCM na ujanja wetu wote huko nyuma hatukumshinda huyu mzee siasa hizi anazijua vizuri simjui mtu wa kumfanananisha naye.
“Nimejiunga na ACT Wazalendo ili kufanya kazi na wanachama wake kushawishi wananchi kwamba chama hiki kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli nchini, ACT ni chama kinachokua kwa kasi kubwa kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania,” amesema Membe.
Aidha, Membe amesema kuwa alifukuzwa na CCM kutokana na msimamo wake wa kuikosoa serikali na kuonyesha nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2020 .
Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni mgombea urais kwa upande wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, amemuomba Membe achukue fomu na kugombea urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo.
Ikumbukwe Julai 6 mwaka huu Membe alirejesha kadi ya uanachama ya CCM. Kiongozi huyo wa zamani alirudisha kadi ya uanachama ingawa CCM ilishamfukuza uanachama
No comments :
Post a Comment