dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 20, 2021

Hasira ni Faida (Hasira Chanya), Hasira ni Hasara (Hasira Hasi). Jua namna ya kuzipambanuwa!

by an unknown author

Hasira ni hisia za kawaida za binadamu ambazo kwa namna moja ama nyingine zaweza kuwa ni zenye afya na manufaa hasa wakati zinapoegemea kwenye upande chanya. Kwa mfano, hasira inaweza kuwa na faida ikiwa itamfanya mtu aazimie kushinda vizuizi au matatizo fulani. Vilevile, hasira inaweza kuwa ni hatari na haribifu wakati inapokuwa nje ya udhibiti wetu.

Hasira yaweza kukudhuru na kukufanya uwe na uchungu au kukufanya useme mambo yenye kuumiza utakayojutia hapo baadaye. Mara nyingi hasira huleta hasara badala ya faida. Kunahitaji kubwa sana la kujifunza namna ya kudhibiti hasira zetu badala ya kuruhusu hasira zitudhibiti.

SHULE YA KUDHIBITI HASIRA HASI👇👇

Kufanya Mazoezi ya Kutafakari

Wakati tunapohisi  kupandwa na hasira  ni muhimu tukajizuia  na kutafakari kuhusiana na hasira zetu kwa kujinenea wenyewe.

Unaweza ukajiambia “Hasira hii haitonisaidia kwa namna yoyote. Hasira hii itafanya hali kuwa mbaya zaidi”. Hata kama sehemu fulani ndani yetu itabaki kuwa na hasira, lakini kwa kujinenea maneno hayo kutatusaidia katika kutuweka mbali na hisia za hasira Hasi.

Kufanya mazoezi ya kutabasamu. 

Njia nyingine na iliyo rahisi ya kuondokana na hasira ni kufanya mazoezi kutabasamu. Mwanadamu anapaswa kutabasamu kabla ya kulala na baada ya kuamka angalau mara tatu kwa wiki.Hakuna kitu  chenye nguvu kama tabasamu. Tabasamu halikugharimu chochote. Unapokuwa unatabasamu unakuwa unaondoa na kufuta hisia zote zilizo hasi ikiwemo hasira hasi.

Support This Blog On Patreon: https://www.patreon.com/zanzibarnikwetu

Jifunze kukaa kimya unapokuwa na hasira hasi. 

Hii ni njia muhimu ya kuondokana na hasira pamoja na madhara yatakayo ambatana nayo. Ni jambo la busara kutokuzungumza chochote unapokuwa umekasirika. Kwa kuzungumza huku ukiwa ni mwenye hasira hasi kunakuza majibizano, malumbano, kutokuelewana, na kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kupeleka kuumiza hisia za wengine. Unapozungumza huku ukiwa na hasira, unakuwa unazidisha chuki na hasira kutoka kwa wengine. Lakini kama utajizuia na kukaa kimya utakuwa unaruhusu kuondoka kwa hisia za hasira hasi.

HERI YA MWAKA MPYA WALIMWENGU.......Mwaka ndo Umeanza,  Badilisha fikra zako leo, Thamini amani kuliko hasira hasi. 

Hali yetu ya kutokuwa wakamilifu inafanya iwe vigumu zaidi kwetu  kuepuka hasira na matendo ya hasira. Lakini licha ya hivyo yatupasa kutambua kwamba; hasira isiyodhibitika inaweza kutufanya tufanye mambo ambayo tutakuja kuyajutia baadaye. Kuwa na hasira ni jambo la kawaida, ila ni muhimu tukajifunza kuthamini amani kuliko hasira. Na hii itatusaidia katika kuondokana na hasira.


No comments :

Post a Comment