dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 31, 2021

Janeth Magufuli : Mfahamu mke wa aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli!

  • Rais wa Tanzania John Magufuli na mkewe Janeth walifunga ndoa ambayo haikuambatana na sherehe.
Mama Janeth Magufuli ana rekodi ya aina yake. Yeye alikuwa 'First Lady' wa tatu kuitwa Janeth katika nchi hiyo ya Afrika mashariki akitanguliwa na Janet au Janeth Museveni (Mke wa rais wa Uganda Yoweri Museveni) na Jeaneth au Janeth Kagame (Mke wa rais wa Rwanda Paul Kagame).

Mke huyo wa rais Magufuli alipokea kijiti cha kuwa 'First Lady' kutoka kwa Salma Kikwete.

Kitaaluma ni mwalimu ambaye alifundisha Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam katika masomo ya Jiografia, Tehama na Historia.

Mama Janeth Magufuli amesoma shule ya msingi Mbuyuni kisha akawa mwalimu shuleni hapo kwa miaka 17.

Tarehe 18 Februari mwaka 2016 aliwaaga wanafunzi wa shule hiyo ili kuanza majukumu ya kuwa mke wa rais.

Shule hiyo ina rekodi ya kipekee nchini Tanzania kwa kuwatoa wake wawili wa marais; mke wa rais mstaafu Jakaya Kikwete na John Magufuli.

Salma Kikwete naye alifundisha katika shule hiyo wakiwa chini ya Mwalimu Mkuu Dorothy Malecela.

Janeth Magufuli ana umri wa miaka 61 na hakuonekana hadharani kwa siku nyingi.


Ni mwanamke mkimya, haiba yake haifanani na watangulizi wake Salma Kikwete, Anna Mkapa wala Sitti Mwinyi. Kwa mbali Mama Janeth amefuata nyayo za Mama Maria Nyerere ambaye hakufanya harakati zozote za siasa wakati mumewe Mwalimu Nyerere akiwa madarakani.

Salma Kikwete amekuwa akijihusisha harakati za maendeleo ya watoto wa kike nchini Tanzania kama ilivyokuwa kwa Mama Anna Mkapa aliyejihusisha na shughuli mbalimbali zilizogusa siasa kwa namna moja au nyingine.

Salma Kikwete aliingia kwenye hekaheka za kisiasa ndani ya CCM akiwa miongoni wa wajumbe mkoani Lindi na baadaye aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge kisha muda wake ulipomalizika aligombea moja kwa moja jimboni na kushinda katika uchaguzi mkuu 2020.

Mama Janeth hana dalili za kuingia kwenye siasa hata kwa kipindi ambacho mumewe alikuwa mbunge, waziri hadi Amiri Jeshi Mkuu.

Aidha, mke wa rais ni cheo kisicho rasmi kinachoshikiliwa na mke wa Rais wa Tanzania, tangu zamani wake wa marais huanza kwa kuitwa mama. Miaka ya karibuni kulikuwa na mijadala mingi kuhusu suala la kuongeza umaarufu wa wake za marais wa Tanzania. Kumekuwa na mapendekezo pia na kupelekwa bungeni kwa nia ya kurasimisha Ofisi ya Mke wa Rais.

Nilifunga ndoa bila koti la suti, mke wangu bila gauni la bi harusi

JANETH MAGUFULI - Aliyekuwa mke wa kwanza wa Rais John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania John Magufuli alisema kwamba alifunga ndoa bila kuvaa koti la suti na mkewe Janeth hakuvaa gauni la bibi harusi.

Ndoa hiyo ilifungwa wakati Magufuli akiwa mwanafunzi katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na haikuambatana na sherehe yoyote.

Akiongea katika mdahalo uliofanyika UDSM kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake wa nchi, Magufuli alisema alifurahi kurudi chuoni hapo ambapo si tu alipata elimu yake ya juu bali kufunga pingu za maisha.

"Siku niliyooa watu wengi hawakujua…na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana."


"Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padre, tena zilikuwa za shaba. Padre pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunywa pepsi na mke wangu alikunywa mirinda...Baada ya hapo nikaenda zangu lab (maabara) kuendelea na shughuli zangu."

Padre ambaye aliwafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwa mujibu wa Rais Magufuli anaitwa Msemwa na sasa yupo Tanga. "Mfuateni father (Padre) Msemwa yeye atawaeleza vizuri zaid."

Magufuli pia amesema hata ndoa za watoto zake haziambatani na sherehe kubwa, "mpaka sasa watoto zangu watatu wameshafunga ndoa na sikufanya sherehe kubwa. Mmoja alifunga ndoa tayari nikiwa madarakani lakini wala hamkusikia."

Magufuli akimjulia hali mkewe alipolazwa hospitali ya Muhimbili Novemba 2016

Novemba 2016 mke wa Rais Magufuli aliugua na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hatua hiyo iliwashangaza wengi ambao walitarajia labda angepelekwa nje ya nchi kama ilivyokuwa ada ya vigogo pale walipofikwa na maradhi.

Toka alipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita Rais Magufuli amekuwa mashuhuri ndani na nje ya Tanzania kwa hatua zake za kubana matumizi yasiyo ya lazima. Tukio hilo la harusi, ambalo ni la maisha yake binafsi linatoa mwangaza wakuelewa ni kwa nii Magufuli hatetereki katika kubana matumizi ya serikali yake.

Mwezi mmoja toka alipoingia madarakani alifuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania kwa mwaka 2015 na kuagiza mabilioni ya fedha yaliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hizo kutumika kujenga kipande cha barabara moja iliyokuwa sugu kwa foleni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya hatua kali alizozichukua katika kupunguza matumizi ya serikali ni kuratibu safari za nje za watumishi ambapo kwa sasa lazima mtumishi apate kibali ndipo asafiri nje. Hata yeye mwenyewe bado hajasafiri kutoka nje ya Afrika.

Yeye mwenyewe ametembelea nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia tu, tangu alipoingia madarakani.

Posho za vikao vya watumishi zimepunguzwa na nyengine kuondolewa kabisa, huku kumbi za mikutano zikitakiwa kuwa ni za serikali tu.

No comments :

Post a Comment