Aliyefungua kesi Mahakamani kuhusu uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka 🇹🇿.
Anaitwa Ally Saleh, ni muandishi wa habari mkongwe aliyewahi kufanya kazi (BBC), pia ni mbunge mstaafu wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Zaidi, pia alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa Urais wa (TFF) walioenguliwa kwa kile kilichoelezwa kuwa hawana vigezo.
Amefungua kesi kwenye mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam na mahakama imesitisha uchaguzi huo huku ikiwaita Rais wa (TFF) na maofisa wengine wanaohusika na uchaguzi huo.
Mahakama imewaita wajieleze ikiwa hoja zao hazitakuwa na mashiko uchaguzi huo utafutwa huku taratibu za kimahakama zikichukua mkondo wake.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
No comments :
Post a Comment