Jhikoman ameweza kukonga nyoyo mashabiki hao ambapo alitumia zaidi ya saa moja jukwaani kwa kupiga nyimbo mbalimbali ikiwemo za zamani na za sasa ambazo zimeweza kufanya vizuri.
Miongoni mwa nyimbo alizopagawisha jukwaani ni pamoja na Afro Caribbean beat, Bad mind, Mpenzi, Ukipendwa, Moto,Mara ya kwanza na nyingine nyingi zikiwemo alizomuenzi msanii Bob Marley katika wimbo wa Hiden.
Wimbo wa Kuagana ambao alimalizia shoo yake hiyo, uliwezakushika hisia za mashabiki wa muziki wa rege waliofurika ambapo walitaka kurudiwa kwa wimbo huo.Mashabiki wa muziki wa rege walionesha hali ya kufurahia muziki mzuri wa rege huku wakiomba Jhikoman arejee kwa mara nyingine siku ya mwisho ambayo ni usiku wa leo wa 7 Agosti.
Mbali na mwanamuziki Jhikoman na Afrikabisa, pia kundi la muziki wa kutoka Zanzibar la Tara jazz waliweza kutoa burundani ya aina yake ikiwemo ufundi wa hali ya juu ya kuchezea ala za muziki wa asili wa jazz wakichanganya vionjo vya muziki wa rege pia walikuwepo wasanii wengine wakiwemo Ras Jamaiel ambaye nae aliwasha moto kwenye jukwaa hilo.
Tamasha la rege Zanzibar msimu huu ni wa tatu tokea kuanzishwa kwake ambapo kila mwaka linakuja kitofauti ikiwemo wasanii wakubwa kutoka mataifa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tamasha hilo, Saidi Omary maarufu kama Saidi Side Rasta, alisema kuwa wasanii wakubwa na bendi kutoka Mataifa zaidi ya 6 wamekuja kwa mara ya kwanza kutoa burudani ya muziki huo.
Nchi hizo ni pamoja na Jamaica, Ubelgiji, Marekani, na zingine ikiwemo Tanzania Bara na bendi za kutoka Zanzibar.
No comments :
Post a Comment