dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 17, 2021

Uganda kuwapokea wakimbizi 2000 wa Afghanistan!

Uganda imesema kuwa itawachukua wakimbizi 2000 wa Afghanistan wanaokimbia mzozo nchini mwao – kufuatia ombi la Marekani.

Hii inafuatia hatua ya wanamgambo wa Taliban kuchukua uongozi wa nchini hiyo wikendi iliyopita baada ya serikali iliyokuwa madarakani kuanguka.

Uganda imepongezwa kimataifa kutokana na sera yake ya kuwakaribisha wakimbizi.

Kundi la kwanza la karibu Waafghanistan 500 linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe saa chache zijazo.

Waziri wa Wakimbizi wa Esther Anyakun ameiambia BBC kwamba Rais Museveni amekubali kuwachukua jumla ya wakimbizi 2000 raia wa Afghanistan – kufuatia ombi la Marekani.

Aliongeza kuwa watakapofika watafanyiwa vipimo vya corona na kuwekwa karantini. Vifaa na gharama zote zitashughulikiwa na Serikali ya Marekani.

Uganda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwapokea watu wanaotoroka ghasia nchini Afghanistan
.

Ug
anda ambayo imekuwa na historia ya muda mrefu ya kuwakaribisha wakimbizi - kwa sasa ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia mzozo na majanga.

Wakimbizi nchi humo wanaoishi katika makazi au vijijini na wenyeji. Baadhi yao wamepewa kipande cha ardhi na kuruhusiwa kufnaya kazi.

No comments :

Post a Comment