dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 9, 2021

JENERALI ULIMWENGU USING IRONY SARCASTICALLY WARNS US ALL!

ABOVE: JENERALI ULIMWENGU - AS THE NAME SUGGESTS , HE IS A REAL ARMY GENERAL OF THE WORLD!

"AU" IACHE UJINGA !

#Jenerali Ulimwengu

Mwanasiasa na mwandishi wa habari mkongwe nchini ndugu Jenerali Ulimwengu amesema Umoja wa Afrika (AU) uache ujinga kwa kuendelea kutetea viongozi ambao wamekuwa wakikandamiza wananchi wao na kudhulumu haki zao.

Jenerali ameyasema haya wakati akizungumza na BBC jana usiku wakati akitoa maoni yake juu ya tukio la kupinduliwa kijeshi kwa aliyekuwa rais wa Guinea ndugu Alpha Condé.

Jenerali amewalaumu AU kwa kukaa kimya wakati rais Condé alipokuwa akifanya matendo ya ukiukwaji wa haki za raia wake na kubadili katiba ya nchi ili kujinufaisha yeye binafsi. Katika uovu wote huu Umoja wa Afrika hawakuwahi kumwonya wala kumkemea bwana Condé.

Kwa hiyo kitendo cha AU kujitokeza na kulaani tendo la kupinduliwa kwake na jeshi la nchi hiyo kimeufanya Umoja wa Afrika kudhauliwa na watu wote.

Katika hili Jenerali Ulimwengu amesema "AU iache Ujinga !"

Jenerali ametumia fursa hii pia kuzionya nchi zingine za Afrika ambazo viongozi wake wamezidi kuwaonea raia wao huku wakiendelea kuvunja kwa wazi haki za kiraia na kidemokrasia za nchi zao. Amesema kama Afrika isipobadilika basi mwenendo huu wa majeshi ya nchi za Afrika Magharibi kupindua marais wa nchi zao ili kuwanusuru wananchi dhidi ya ukandamizwaji unaofanywa na viongozi wao utaenea mara moja katika nchi zote za Afrika.

Mapema siku mbili kabla mimi binafsi niliukemea Umoja wa Afrika kwa kuufananisha na "Genge la Wahuni !"

Natarajia watu wengi zaidi watazidi kujitokeza na kulaani mwenendo huu wa AU ambao kiuhalisia umejikita katika kulinda maslahi na mamlaka za marais wa nchi za Afrika pasipokujali ukandamizwaji wa haki za kiraia na kidemokrasia unaofanywa na viongozi hao.

Tunahitaji mwelekeo mpya wa jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU), mwelekeo utakaoonesha kujali maisha na maslahi mapana ya wananchi kwanza badala ya kuendelea kutetea ubinafsi na matendo ya kidikteta  ya marais wa Afrika dhidi ya raia wa nchi zao.

#Modest Alphonce


No comments :

Post a Comment