Abdulrazak Gurnah ambaye ni mwandishi wa riwaya kutoka Zanzibar amekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo la fasihi ‘’ kwa kuangazia athari za ukoloni na hatma ya wakimbizi katika ghuba baina ya tamaduni na mabara.
Tuzo hiyo ilitolewa na taasisi ya Uswizi ya Nobel na ina thamani ya pesa za Uswizi crowns milioni 10 sawa na dola milioni 1. 14.
Gurnah ambaye alizaliwa Zanzibar katika mwaka 1948, aliwasili Uingreza kama mkimbizi katika miaka ya mwisho ya 1960.
Ni muandishi wa riwaya 10 na hadithi kadhaa fupi fupi. Alikuwa Profesa wa Kiingereza na fasihi ya baada ya uhuru katika Chuo kikuu cha Kent, Canterbury, hadi alipostaafu.
Gurnah, mwenye umri wa miaka 73, ni mwandishi wa riwaya 10, ikiwa ni pamoja na Paradise na Desertion.
Paradise, riwaya iliyochapishwa katika mwaka 1994, ilielezea hadithi ya mvulani aliyekulia nchini Tanzania mapema mwanzoni mwa karne ya 20 na kushinda Tuzo ya mwandishi wa kitabu, mafanikio aliyoyapata kama mwandishi wa riwaya.
"Kujitolea kwa Abdulrazak Gurnah kuangazia ukweli nan a kutopenda urahisishajini jambo lililovutia na kufurahisha," Kamati ya Nobel kitengo cha fasihi ilisema katika taarifa yake.
"Riwaya zake ziliangazia kuanzia ubaguzi ufafanuzi wa ubaguzi na kuweka wazi Afrika mashariki yenye watu mbali mbali ambayo wengi katika maeneo mengine ya dunia hawaifahamu."
"Wahusika wake wanajipata katika hali ya mkanganyiko kwa kuwa baina ya tamaduni na mabara, baina ya maisha waliyokuwa nayo kipindi cha nyuma na maisha yanayojitokeza, ni hali ya kutojihisi salama ambayo haiwezi kutatulika’’
Gurnah ni mwandishiMwafrika wa kwanza mweusi kushinda tuzo hiyo tangu aliposhinda Wole Soyinka katika mwaka 1986.
Tuzo za Nobel, ambazo zimekuwa zikitolewa tangu 1901, zinatambua mafaniko katika fasihi, sayansi, amani na uchumi.
Waandishi wa riwaya walioshinda katika nyakati zilizopita ni kamaErnest Hemingway, Gabriel Garcia Marquez na Toni Morrison, riwaya kama Pablo Neruda, Joseph Brodsky na Rabindranath Tagore, na waandishi wa mchezo akiwemo Harold Pinter na Eugene O'Neill.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill alishinda katika kitengo cha kumbukumbuza kihistoria na Bertrand Russell kwa falsafa yake na Bob Dylan kwa maandishi ya muziki wake.
No comments :
Post a Comment