Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 17, 2021

BARAKA SHAMTE AMKAANGA DR. AMANI ABEID KARUME!

  • Shamte aitaka ccm kumfukuza Dkt Karume.
Zanzibar's former President Dr. Amani Abeid Karume

The flamboyant Baraka Mohamed Shamte

Mwanasiasa mkongwe Baraka Mohamed Shamte amesema ccm kinapaswa kujifunza kuteua wagombea urais wenye msimamo dhaifu kama ulioonyehwa na Rais Mstaafu Dkt Amani Karume kwenye kongamano la kukumbuka mchango wa kusaka mapatano uliotolewa na hayati Maalim seif sharif Hamad.

Pia amekitajwa kilichosemwa na rais huyo mstaafu kwenye hotiba yake ni zaidi usaliti ambao hautamfaa wala kumkinga na mambo mabaya alioyoyafanya wakati akiwa madarakani toka mwaka 2005 hadi 2010.

Msimamo huo umetolewa jana na baraka shamte katika mahojiano na Gazeti hili yaliofanyika nyumbani kwake ndani ya mji mkongwe wa zanzibar hukp mkunazini katila manispaa ya jiji la zanzibar kisiwani hapa.

shamte alisema inasikitisha sana kumsikia Dkt karume akimtupia lawama aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu hayati Mzee Idrisa Abdul Wakil kwa kuvunja Baraza la mawaziri na kumuondoa maalim Seif kwenye nafasi ya uwaziri kiongozi smz bila Dkt karume kutaja mikasa ya maalim seif dhidi ya Mzee wakil.

Alisema hayati Mzee Wakil alimfukuza maalim Seif na kumteua Dkt Omari Ali Juma kwa sababu ambazo Dkt Karume anazijua kwani wakati akiwa rais wa zanzibar amewahi kumshutumu maalm seif na kumwita kiongozi mkorofi aliyekuwa akisakamwa na tamaa ya kutaka madaraka lwa pupa.

Aidha alisema vile vile Dkt karuma anajua pia uchonganishi ulifanywa na maalim Seif kwa Rais jukius Nyerere hadi mzee Aboud Jumbe akavuliwa madaraka yake lakini cha ajabu leo ulimi wake ameugeuza na kutamka kinyume chake.


"Inasikitisha kumsikia Dkt Karume leo akiita dodoma kwa kebehi na dhihaka wakati ndipo mahali alipohurumiwa na kiteuliwa kuwa Rais. Hapa Zanzibar kwenye kamati maalum alipata kura tisa na akipitwa na wagombea wengine.Tunajua amekuwa Rais na kutajirika acha akidhihaki chama kilichombeba hadi akawa rais" "Alisema shamte.

Alisema hakikuwa kitendo cha kiungwana kuyazumgumzia maisha ya maalm seif kwa kutaja mema yake na kuzilwepa dosari na kasoro zake kwani ndiye aliyewahasimisha wananchi wa pemba na umguja na lufikoa kuishi maisha ya uadui na chuki.

"Dkt Karume tumaisikia hotuba yake iliothibitisha sasa si mwanaccm tena. Kwa muda mrefu alijificha na sasa mungu amembainisha .CCM kitafanya makosa makubwa kikiendelea kumuamini na kudhani ni mwenzetu .Kama kinasubiri yatokee mambo kadha wa kadha kitajuta" Alieleza shamte.

Alisema kabla ya rais wakil kumteua maalim seif kuwa waziri,akawa mjumbe wa nec na ccm,zanzibar hapakuwa na mpasuko wowote lakini tokea aliposhindwa kira za urais ndani ya chama na kufukuzwa ccm ndipo mpasuko na mgawanyiko wa kisiasa ulipoanza.

Jaibu katibu mkuu wa ccm zanzibar Dkt Abdallah Sadalah Mabodi alipoulizwa jana kuhusiana na hotuba ya dkt karume alisema hayupo kwenye nafasi nzuri ya lulizumgumzia suala hilo hadi wakati mwingine muafaka baada ya vikao vya juu vya chama kukutana.

Dkt Mobodi alisisitiza kuwa ccm haijawahi kutochukua hatua zozote ngumu kwa maslahi au kwa mustakabali wa ustawi na uhai wa chama hicho tawala.

No comments :

Post a Comment