Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 17, 2021

Kesi ya Mbowe: Jaji Tiganga atoa uamuzi wenye ukakasi. Aahirisha kesi mara tatu!

  • Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo tarehe 17 Novemba 2021.

Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anatambulisha

  1. Pius Hilla
  2. Abdallah Chavula
  3. Nassoro Katuga
  4. Jenitreza Kitali
  5. Tulimanywa Majige
  6. Esther Martin
  7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha mawakili wa utetezi

  1. Jeremiah Mtobesya
  2. John Mallya
  3. Dickson Matata
  4. Idd Msawanga
  5. Seleman Matauka
  6. Hadija Aron
  7. Evaresta Kisanga

Jaji anawaita washitakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne. Wote wapo.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi mdogo. Tupo tayari.

Peter KIBATALA: Na sisi pia tupo tayari kuendelea kusikiliza uamuzi na kuendelea na shauri.

JAJI: Ni kweli kwamba mahakama hii iliahirisha shauri kwa ajili ya kusoma uamuzi, na uamuzi upo tayari, na haya ndiyo maamuzi yenyewe. Kwenye shauri maarufu sana la Uingereza, aliyekuwa Jaji Mkuu wa Uingereza wakati huo alitoa kauli ambayo inaishi mpaka leo, kwamba haki siyo tu itendwe bali ionekane Ikitendwa. Na kauli hiyo imekuwa ikitumika mpaka leo pamoja na shauri hili kuwa tofauti. Kwa mtu atakayesoma uamuzi huu hataelewa kwanini nimefika uamuzi huu.

JAJI: Historia inaonyesha askari polisi mwenye Namba H4323 DC Msemwa alipokuwa anatoa ushahidi wake mahakamani aliomba kutoa kielelezo chake. Wakati anatoa upande wa utetezi walipinga. Na wakati pande zote mbili wakieendelea kutoa hoja, basi Wakili Peter Kibatala alisimama na kusema kwamba anaomba kui- move Mahakama kwamba shahidi aliyepo kizimbani ana diary, pen na simu, na kwamba aliomba kwamba Mahakama itamke kwamba siyo shahidi tena na kwamba ushahidi uake ufutwe wote. Mahakama ilichukua vitu vile na kwa sababu muda ulikuwa umekwenda sana, Mahakama ilishindwa kulishughulikia jambo lile.

JAJI: Na mpaka ilipofika (Novemba) 15 Mahakama ilianza kujiridhisha kwamba kama ingeweza kujiridhisha kwa kushughulika simu … Hata hivyo Mahakama ikaona hakuwa akitumia simu yake basi Mahakama ikaona arudishiwe simu yake. Na Mahakama ikabakia na diary na pen. Hata hivyo, Mahakama ikawaelekeza mawakili kwamba wakafanye utafiki. Itakapofika tarehe 15 waje na utafiti. Ilipofika siku ya tarehe 15 Mahakama ilishughulikia suala la uamuzi kwanza kwamba Mahakama ilielekeza kielelezo kipolewe na kisomwe.

JAJI: Lakini kabla ya Mahakama haijasoma kielelezo hicho basi Mtobesya alisimama kabla shahidi hajasoma akaomba Mahakama isikilize jambo hilo kabla shahidi hajasoma kwa sababu akisoma itaonekana aliendelea kutoa ushahidi. Upande wa mashitaka wakasema hawana pingamizi. Wakati hoja inaleta walisema kwamba waliona jambo hilo wakati Mahakama inaendelea. Wakasema kwamba shauri linaundwa juu sheria ya Uhujumu Uchumi lakini wakaona sheria hiyo haisemi moja kwa moja. Basi kwa kutumia kifungu hicho cha 28 na 264 ndiyo lilijenga misingi kwa wao kuleta jambo hilo. Wakasema kwamba shahidi anapokuwa kizimbani hatakiwi kuwa na nyaraka yoyote na kwamba wakaomba Mahakama itamke kwamba shahidi hafai na ushahidi wake ufutwe. Wakasema kwamba kuna sheria mbalimbali zinazoelekeza jambo hilo kama 168 ya Uhujumu Uchumi na PGO ya 282. Lakini Kifungu cha 28 cha sheria hiyo kinaipa mamlaka Mahakama kutumia sheria nyingine. Basi wakatumia Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu cha 264.

JAJI: Walitoa hoja mbalimbali. Kwa sababu ya muda sitazitaja zote. Nitaje Kesi walizotumia wakati wa shauri hili kama Nanyaro vs Peniel, Edward Isack Shayo vs Jamhuri, Okumu vs Uganda, Goodluck Kyando vs Jamhuri. Zote zimetumika katika kutoa uamuzi huu.

JAJI: Msingi wa hoja yao kwamba shahidi hatakiwi kuwa na kitu chochote wakati Mahakama ikiendelea bila kuwa na kibali cha Mahakama, ukweli ni kwamba walimuona shahidi wakati hoja zingine za mawakili wa Serikali wakizitoa. Hakuna ushahidi kwamba alikuwa akirejea jambo lolote.

JAJI: Kwa sababu hiyo waliiomba mahakama i- presume mambo yafuatayo kwamba wakati anaingia kwenye kizimba hicho aliingia nayo. Kwamba material ambayo aliingia nayo wakati Mahakama aikiendele ionekane alitumia kwa sababu aliingia na nyaraka bila kibali cha Mahakama basi shahidi aonekane ni incompetent.

JAJI: (Kwamba) Ushahidi ambao ameshautoa haufai na aondolewe kutoa ushahidi Mahakamani. Na kama itaonekana kwamba suala la kumwondoa shahidi ni gumu basi wakaomba Mahakama iruhusu notebook kukaguliwa na wao wapewe ili waweze kutumia notebook hiyo katika maswali yao.

JAJI: (Kwamba) Kanuni inakataza shahidi kuingia na nyaraka kizimbani, Quran tukufu na Biblia tukufu ndiyo vitu pekee vinavyoruhusiwa kuingia navyo Mahakamani. Kwamba kwa shahidi kuingia na mambo mengine yanafanya shahidi asiaminike. Mahakama ikaombwa imkoseshe sifa shahidi kwa kutumia kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi. Kuhusu hilo upande wa mashitaka walipinga kwamba vifungu hivyo siyo wezeshi.

JAJI: Mahakama kwa upande wake ikaona ianze na vifungu hivyo kama ni vifungu wezeshi au siyo wezeshi. Kufungu cha 127 kinasema Mahakama Kuu inayo mamlaka katika kutekeleza majukumu yake kuweka taratibu juu ya kuendesha majukumu yake ya jinai. Kifungu kilimaanisha kuisaidia Mahakama katika kufanya jambo lolote ambalo sheria haijaeleza.

JAJI: Kwamba kama sheria halijaweka taratibu basi kifungu hicho cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaipa mamlaka kwa Mahakama kushughulikia, na kwamba kwa sababu jambo lenyewe lilitokea wakati shauri likiendelea, basi upande wa utetezi wapo sahihi kwamba kifungu hiki kinaipa Mahakama mamlaka. Jambo la pili kwamba kwa kutumia kifungu cha 127 walesma kwamba mahakama itamke kwamba Shahidi hafai na ushahidi wake ufutwe. Kwa sababu hiyo nasoma kifungu hiki.

(Jaji anasoma).

JAJI: Ukisoma kifungu hiki kinaweka vigezo ambavyo ni wazi vinaweza kufanya Shahidi asitoe ushahidi wake mahakamani. Kwa sababu hiyo naona kwa kifungu hiki upande wa utetezi wametaja kifungu sahihi bila kujali kama wapo sahihi ndani yake kuhusu shahidi huyu. Kuhusu sheria kesi ya Edward Isack Shayo vs Jamhuri, haina uhusiano katika kesi hii. Kwa kuwa Mahakama imeli- solve issue ya jurisdiction imelimaliza. Imebakia issue kama shahidi vitu alivyokuwa navyo vinaruhusiwa na Mahakama. Pande zote mbili zinakubalina kwamba shahidi alikuwa na notebook kwenye kizimba na kwamba hata alipoelekezwa aliotoa mwenyewe. Jambo linabakia kwamba je, ni kinyume cha sheria kwa shahidi kuingia na notebook kwenye kizimba? Na kwamba upande wa utetezi wanasema siyo taratibu na upande wa mashitaka wanasema ni sahihi.

JAJI: Utetezi walisema tungalie sheria ya PGO ambapo inaruhusu askari polisi ambaye ni shahidi kuingia na notebook kwa ruhusa ya Mahakama. Na kwamba anaweza kujikimbusha kwenye notebook baada tu ya kuruhusiwa na Mahakama. Nakubalina na upande wa mashitaka kwamba shahidi anaruhusiwa kuingia na notebook kwenye kizimba cha Mahakama. Kwamba hakuna sheria ya moja kwa kwa moja inakataza shahidi kuingia na notebook kwenye kizimba cha Mahakama. Jambo linalobakia kwamba ni kama shahidi alitumia notebook.

JAJI: Mtakumbuka mshitakiwa ambaye hana wakili anaruhusiwa kuingia na vielelezo kwenye kizimba. Kwa hiyo shahidi ambaye anatoa ushahidi anaweza kuingia na kielelezo mpaka muda atakapoomba kutumia. Hili linaungwa mkono na Sheria ya Ushahidi katika kifungu 168(1,2) ya Sheria ya Ushahidi.

JAJI: Kwamba shahidi yeyote anapokuwa anaendelea kutoa ushahidi mahakamani ataruhisiwa kufanya ukumbusho. Na kwamba wakati anaandika hiyo nyaraka alikuwa na kumbukumbu wakati huo. Na kwamba aliposoma andiko hilo lilikuwa sahihi. Basi ukisoma PGO 282 (7) A & A na Sheria ya Ushahidi kifungu cha 168 1 na 2 shahidi hakatazwi kuingia na kitu chochote kwenye kizimba, na kwamba kabla hajafanya marejeo ataomba ruhusa ya Mahakama.

JAJI: Jambo linalofuatia katika shauri hili, ni wazi hakuna kilichoonekana kama shahidi akiwa anafanya rejea. Nakubalina na Kibatala na Mtobesya kwamba hayo yalifanyika wakati shahidi ana kiapo chake. Sheria inasema kwamba wakati amefungua alikuwa anafanya nini. Mahakama inaona ni kweli kwa yeye kufungua na kuandika ilikuwa ni violation. Jambo linalofuatia ni je, baada ya violation Mahakama ione nini kitaifuata. Upande wa utetezi wakasema baada ya violation wanaomba atamkwe hafai na ushahidi wake ufutwe.

JAJI: Kuhusu kumtoa shahidi asiendelee kuwa shahidi sheria inasema ni shahidi ambaye hana uwezo wa kujibu maswali na kwamba iwe imesababishwa na umri mkubwa au mdogo. Upande wa utetezi wameomba itumike hiyo ya mwisho ya ‘any other similar cause’. Mahakama imeombwa kurejea kwenye andiko ambalo Mr Kibatala alilirejea hapa Mahakamani akiwa ameichukua kutoka North Carolina, kwamba moja ya mambo kwao ni pale shahidi anakosa sifa ni kwa shahidi kukosa kuona umuhumimu wa kutoa ushahidi wake.

JAJI: Kwa sababu hiyo sheria hiyo kwetu Tanzania hakuna. Mtobesya ameiomba mahakama ifanye kazi ya Bunge. Mahakama haiwezi kuongezea jambo hilo pamoja na kuomba kwamba Mahakama inaweza kuongezea sheria hiyo pale ambapo inaona kwamba kuna ulazima wa kufanya jambo hilo.

JAJI: Hasa ikiwa imethibitishwa kwamba kweli limetokea suala la kwamba shahidi hajaona umuhimu wa kuzungumza ukweli kwa kuwa hakuna sehemu imeelezwa kwamba shahidi hajui umuhimu wa kuzungumza ukweli. Kinachoonekana ni kwamba shahidi kwa kuonekana na jambo hilo mahakamani ni suala la kutoaminika ushahidi wake. Mahakama hii sasa inashimdwa kumuodoa shahidi huyu … Nafahamu katika PGO ya 292 (5&6) imeeleza sifa ya notebook na kwamba details za namna gani kwamba inatakiwa kuwa na taarifa za utendaji kazi.

JAJI: Hapo ndipo nakubalina na suala la utetezi kwamba upo umuhimu wa kukagua notebook hiyo. Lakini Mr Chavula alisema kuwa si wote ambao wanaruhusiwa kukagua notebook hiyo kwa PGO 282 (7)C kwamba ndiyo kuna watu waliotajwa kuhusu kukagua notebook hiyo.

JAJI: Lakini kwa jambo hilo Mahakama ina maamuzi kwamba nyaraka yoyote inayojitokeza kwenye mwenendo wa kesi mahakamani basi itakuwa ni nyaraka ama kielelezo cha Mahakama. Na kwamba kwa sababu notebook hiyo ilikutwa kwenye kizimba cha mahakama hii basi upande wa utetezi … Lakini Mahakama ina maoni kwamba kuhusu taarifa za siri zilizokuwa katika notebook hiyo zinaweza kuangukia katika mikono ya watu wasiohusika.

JAJI: Kwa Namna hiyo basi, kwa sababu jambo hilo linahusu haki za watu, Mahakama inaweka utaratibu wa wakili mmoja mmoja ataruhisiwa kukagua na kwa sehemu husika tu. Na wakili hataruhusiwa kupiga picha sehemu ya notebook hiyo.

JAJI: Hiyo ndiyo maana ya kauli yangu kwamba ‘haki isitendeke tu, bali ionekane ikitendeka.’ Na huo ndio uamuzi wangu.

(Mawakili wa pande zote mbili wanasimama kukubaliana na Jaji).

JAJI: Sasa kuhusu utaratibu wa nani ataruhisiwa kukagua, mtachaguana mmoja mmoja, na kwamba notebook hii ilikuwa chini ya mikono ya Mahakama. Basi nawakabidhi hapa.

JAJI: Mniambie maoni yenu mkafanyie zoezi hili katika usiri au hata hapahapa. Nahitaji maoni yenu

(Mawakili wa pande zote mbili wanashauriana).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Kama ukiridhia naomba uahirishe shauri kwa muda kwa sababu hatuwezi kujua ukaguzi utachukua muda gani.

JAJI: Utetezi ni sawa?

KIBATALA: Sawa. Haina Shida. kwa dakika 20 inatosha.

JAJI: Kwa sababu nimesema taarifa yoyote isichukuliwe kwa picha au vinginevyo, basi namweka na afisa wangu mmoja kwa ajili ya kusimamia hilo zoezi.

(Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana kuhusu hilo).

JAJI: Dakika 20 pamoja na maandalizi ya kurudi tufanye saa tano kamili. Basi naahirisha kwa nusu saa.

Jaji amesharejea mahakamani. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa kwa mara nyingine.

Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anamwambia jaji kuwa column yao iko vile vile na kwamba wako tayari kuendelea na shauri.

Wakili Peter Kibatala naye anamwambia jaji kuwa kwa upande wao wako vile vile lakini anaomba kumwongeza Nashon Nkungu ambaye alikuwa Mahakama ya Rufaa.

Anasimama Wakili Mtobesya.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, muda mfupi uliopita tumetoka kwenye zoezi la kukagua diary.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Objection Mheshimiwa Jaji. Hilo haliruhusiwi hata kidogo na hatuko tayari kuona anaendelea. Uamuzi mdogo umeshatolewa.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji sijui niongee nini nisionekane namkosea heshima kaka yangu.

MTOBESYA: Kwamba sisi hatukuwa tumeenda kufanya mchezo wa kitoto na kisha kurejea nyumbani.

JAJI: Nini hasa ulitaka?

MTOBESYA: Nilikuwa nataka kui- move Mahakama chini ya kifungu cha 176 (1) chini ya Sheria ya Ushahidi. Mahakama ikiona inafaa imtake atoe nakala ya nyaraka yake.

JAJI: Sasa mimi sijajua nyie mmeona nini. Labda tuingie ofisini tukaone mmeona nini. Unasemaje Mr Robert Kidando?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Sawa Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Naahirisha kwa muda.

(Jaji anatoka mahakamani kuelekea ofisini kwake).

Jaji amerudi mahakamani na kesi imeshatajwa kwa mara nyingine tena. Ni kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.

Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anasema safu yao iko vile vile kama mwanzo na wapo tayari kuendelea na shauri.

Peter Kibatala naye anasema safu yao haijabadilika na wapo tayari kuendelea na shauri.

Mtobesya anaanza tena.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, wakati umetupatia nafasi ya kwenda kukagua diary tumekuta kuna mambo yapo relevant na kesi yetu. Kwa sababu hiyo kupitia kifungu 176(1) ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 tunaiomba Mahakama tupatiwe kama kielelezo.

JAJI: Upande wa mashitaka?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.

JAJI: Basi hiyo relevant part Mahakama inaelekeza ichukuliwe na iingie kama sehemu ya kielelezo.

(Mawakili wote wa pande zote mbili wanakubaliana).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji kuna shahidi alikuwa anaendelea na ushahidi wake. Tupo tayari kuendelea.

JAJI: Shahidi Karibu.

KIBATALA: Tupo tayari kwa ruhusa yako.

(Shahidi ameshapanda kizimbani).

JAJI: Shahidi nakukumbusha kuwa ulishakula kiapo na kwamba chini ya kiapo hicho utaendelea kutoa ushahidi wako. Kwa mujibu wa taratibu zetu shahidi anatakiwa asome kielelezo, au kuna jambo lingine?

WAKILI WA SERIKALI: Hapana Mheshimiwa.

JAJI: Soma kwa sauti.

SHAHIDI: The United Republic of Tanzania. Registeer … P.o. Box 35069, Dar es Salaam, 0222726451/022926458, W. W. W. Judiciary, Reference number 68/77/01/30, P. o. Box 1733 … Case 16/2021/NPS. 180/TRS/08/2020 /06 ….

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Shahidi barua uliyosoma ni ya tarehe ngapi?

SHAHIDI: Novemba 12, 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Imeandikwa kutoka wapi kwenda wapi?

SHAHIDI: Kutoka kwa Deputy Register wa P.o. Box 35067 Dar es Salaam kwenda NPS Dodoma, P.o Box 1733 Dodoma.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa barua hiyo walikuwa wanamaanisha nini?

SHAHIDI: Kwa barua hii namkabidhi Detention Register DC Msemwa kama ilivyoombwa.

WAKILI WA SERIKALI: Detention Register ipi?

SHAHIDI: Exhibit TP 1.

WAKILI WA SERIKALI: Ukiondoa DC Msemwa wengine ni akina nani?

SHAHIDI: Ni Jaji in charge wa Mahakama hii.

WAKILI WA SERIKALI: Barua ulipokea lini?

SHAHIDI: Tarehe 12 Novemba 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Tofauti na barua hii, Msajili alikukabidhi kitu gani kingine?

SHAHIDI: Detention Register.

WAKILI WA SERIKALI: Detention Register ya mamna gani?

SHAHIDI: Nilitoa mwanzo kama kielelezo na ni ya kituo cha Central Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Ulitoa kama kielelezo? Kielelezo wapi?

SHAHIDI: Kwenye Mahakama hii hii.

WAKILI WA SERIKALI: Unakumbuka ni shauri gani?

SHAHIDI: Shauri hili hili la 16 /2021.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kwamba ni vigezo gani vinatambulisha hiyo Detention Register.

SHAHIDI: Kwamba kuna initial ambayo ni CD kwamba ni Central Dar es Salaam ambayo huwezi kuipata sehemu yoyote pale.

WAKILI WA SERIKALI: Inaelezea nini?

SHAHIDI: Ili mtuhumiwa aletwe pale Central Dar es Salaam lazima awe na ref. namba ya kesi iliyofunguliwa na kwa pale Central ambayo ni CD kwa maana ya Central Dar es Salaam.

SHAHIDI: Na kama kesi haijaanza kupelelezwa (RB) kwa hiyo inaanza CD/RB namba ya kesi, tunamalizia na mwaka. Unaweza kupewa reference kwa kesi iliyoanza kupelelezwa itaanza CD/ badala ya RB itaingia IR/namba ya kesi na utamaliza na mwaka.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kwamba tarehe 12 Detention Register iliyokabidhiwa kwa Msajili utatambuaje.

SHAHIDI: Pale juu kuja PF namba 20. Ili detention niweze kuitambua lazima iwe na PF namba 20, na pale juu lazima pawe na Ministry of Home Affairs. Lazima pasomeke 12/2020.

WAKILI WA SERIKALI: Hiyo 12/2020 inaamnisha nini?

SHAHIDI: Kwamba, zilitumika zingine zikajaa zikapelekwa records na kwamba hiyo Detention Register ni ya 12.

WAKILI WA SERIKALI: Vitu gani vingine vinaweza kukufanya utambue ndiyo DR uliyoleta Mahakamani.

SHAHIDI: Ndani lazima itakuwa na mwandiko wangu. Niliandika … wakati tofauti tofauti wakati nilipangiwa zamu.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu kingine?

SHAHIDI: Lazima itakuwa mwezi wa nane.

WAKILI WA SERIKALI: Jambo lingine?

SHAHIDI: Tarehe saba Agosti 2020 lazima itakuwa na mwandiko wangu sababu walipoletwa watuhumiwa …

WAKILI WA SERIKALI: Wangapi?

SHAHIDI: Wawili Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Ambao ni akina nani?

Shahidi Mohamed Abdilah Ling’wenya na Adam Hassan Kasekwa.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukabidhiwa Detention Register ikawaje?

SHAHIDI: Nafanya kazi Oysterbay Polisi na kwa sababu ni mpelelezi nina sehemu ya kutunza nyaraka zangu. Niliiitunza.

WAKILI WA SERIKALI: Unayo kwa ajili gani?

SHAHIDI: Kutoa ushahidi Mahakama Kuu.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, shahidi ameonyesha uwezo. Kwa ridhaa ya Mahakama tunaomba akabidhiwe. Shahidi tazama nyaraka hiyo. Ieleze Mahakama nyaraka hiyo ni kitu gani?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji nyaraka hii ni Detention Register, kitabu kinachotunza kumbukumbu kwa mahabusu waliofikishwa Central Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama ina husiano gani na wewe?

SHAHIDI: Ina uhusiano na mimi kwa sababu ndiyo nyaraka niliyoitumia tarehe 7 Agosti 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Ina vitu gani inavyotambulisha ni ya Central Dar es Salaam?

SHAHIDI: Kama nilivyosema mwanzoni kwamba detention itakuwa ya 12 /2020. Nikasema itakuwa na PF namba 20, nikasema lazima iwe na maneno ya Ministry of Home Affairs. Ndani kuna mwandiko wangu kwamba tarehe 7 Agosti 2020 nilipokea watuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Unaiomba nini Mahakama kwa nyaraka hiyo?

SHAHIDI: Naomba ipokee kama kielelezo kwamba tarehe 7 Agosti 2020 nilikuwepo Central na nilipokea mahabusu wawili.

(Mawakili wa utetezi wanaikagua na kupitia kurasa zake kwa haraka haraka. Kisha wanasikitika kwa kutikisa vichwa vyao).

Mtobesya anaamka.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, upande wa utetezi tuna pingamizi kwenye kielelezo hiki. Kwa sasa tunaomba tukutane na wewe pamoja na wenzetu. Lakini tunategemea kuweka mapingamizi matatu katika suala la kupokea Detention Register. Ikishindikana basi tutafanya mawasilisho.

WAKILI WA SERIKALI: Ni sawa Mheshimiwa.

(Jaji anainama na kuandika kidogo)

JAJI: Basi tukutane kwenye ofisi yangu. Karani naomba hiyo Detention Register.

(Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama).

Saa 7:57 mchana Jaji amesharudi mahakamani. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 Khalfani ya Jamhuri dhidi ya Khalfan Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe imetajwa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea na tupo tayari.

KIBATALA: Nasi tupo tayari Mheshimiwa Jaji.

MTOBESYA: Naomba kuongelea mapingamizi mawili then kaka yanngu Kibatala ataongeza katika pingamizi la tatu. Pingamizi letu la tatu lipo kwenye kifungu cha 353 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 kama Ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2019. Kimsingi tunasema kwamba nyaraka hii kwa sababu imeshatumika katika shauri dogo kuhusu kesi ndogo ya mshitakiwa namba mbili, ili kutumika mahakamani, basi Mahakama ilitakiwa itoe kitu kinaitwa ‘disposal order’, amri ya kukitoa kielelezo hicho.

MTOBESYA: Na pingamizi letu la pili ni kwamba kielelezo hiki kilishatolewa maamuzi katika Mahakama hii, hivyo Mahakama hii inazuia kukiongelea tena.

MTOBESYA: Na pingamizi la tatu, kwa kuwa hoja ya the issue of admissibility (the issue estople) inazuia Mahakama hii kutumia kielelezo hicho. Kwa hiyo naongelea kwanza hizi tatu.

MTOBESYA: Naanza na pingamizi la kwanza kwanini palitakiwa kuwa na ‘disposal order’. Kifungu cha 353 ndicho kinaongelea masuala ya ‘disposal order’ na ukisoma ‘heading’ kabla ya a kifungu hicho haijaanza kinaonyesha sehemu C kinaongelea ‘disposal exhibit’. Ndiyo TITLE ya juu.

MTOBESYA: Ukisoma kifungu cha kwanza na cha pili kinaongelea kwa ujumla ila hoja yetu inaongelea kifungu cha 3.

(Wakili Mtobesya anasoma kifungu cha 1 & 2).

MTOBESYA: Naomba sasa umakini wa Mahakama uelekee kifungu kidogo cha 3. Na vifungu vingine vyote vinaendelea.

MTOBESYA: Ni mawasiliano yetu kwamba kielelezo chochote ambacho kilishawahi kuingia mahakamani, tunaomba kurejea kifungu kidogo cha 3 ndiyo tunaona kinahusika hapa. Kwa hiyo tunasema kwamba ni amri pekee ya Mahakama hii Ilitakiwa kutolewa kwa ajili ya kielelezo kilichotakiwa kuingia wakati wa kesi ndogo ya mshitakiwa wa pili wakati ule … kuinyima. Na hivyo basi kielelezo kitakuwa hakijamfikia shahidi kwa utaratibu sahihi.

MTOBESYA: Kwa maana hiyo haiwezi sasa kuingia kwenye proceedings kama ambavyo anaomba shahidi huyu kwa sababu palipaswa pawe na amri ya Mahakama kabla ya Msajili hajatoa kielelezo hicho. Kwa maana hiyo ni ombi letu kuwa kisipokelewe kwa utaratibu huo wa kukiuka utaratibu wa kisheria.

MTOBESYA: Hoja yetu ya pili tunawasilisha kuwa ni inakataza kujadili kielelezo hicho katika kesi ndogo ya kesi kubwa. PW1 alishaomba kuingiza kielelezo hicho lakini ilishindikana na Mahakama ilikataa isiwe sehemu ya ushahidi wake. Hata kwenye rulings za Mahakama wakati Inapokea hili suala tulikubaliana kimsingi kwamba taratibu za upokeaji ni ule ule iwe ID au exhibit.

MTOBESYA: Tunaomba tu tusisitize kwamba suala hili ni jurisdictional issue. Tunaomba ichukuliwe kwa uzito huo kwa sababu inaathiri uzito wa Mahakama kwa kutoa maamuzi kwenye jambo hilo.

MTOBESYA: Tunakazia kwa kurejea kesi tatu _BIBI KISOKO MEDARD vs MINISTER FOR LAND, HOUSING AND URBAN DEVELOPMENT PLANNING ANTA.

(Wakili Mtobesya anasoma).

MTOBESYA: Na pia ipo kwenye ukurasa wa 251 aya ya pili kutoka mwisho inaelezea hicho kitu. Kesi ya pili ni kesi ya Theresia Zacharia vs Oscard Rwechengura. Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoketi Dar es Salaam…

(Wakili Mtobesya anasoma…)

MTOBESYA: Mistari mitatu ya mwisho katika ukurasa wa tatu…

MTOBESYA: Ya tatu ni NBC and Others vs Bruno Vitus Swalo. Maamuzi ya Mahakama ya Rufaa iliyoketi Mbea (Civil Appeal). Kwa maana hiyo jambo hili lilihitimishwa kwamba ni ‘FUNTUS OFICIO’. Kwenye maamuzi ilionekana kwamba siyo sahihi kwa kuleta jambo ambalo limeshatolewa uamuzi.

MTOBESYA: Kwamba kwa kielelezo ambacho shahidi wa pili annaomba mahakama kukitolea mahakama ikatae hicho kielelezo. Na kwa sababu hiyo naomba kumkaribisha kaka yangu Peter Kibatala.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, naomba kuunga mkono hoja zilizotolewa na kaka yangu Mtobesya. Ni suala la utaratibu kwamba kielelezo kinachokuwa chini ya Mahakama kufika kwa shahidi au kwa mtu mwingine ni baada ya Mahakama kutoa maelekezo kwa kutumia ‘DISPOSAL ORDER’.

KIBATALA: Na ‘DISPOSAL ORDER’ zipo za namna mbili. MOJA, ile inayotolewa baada ya shauri kumalizika, na PILI, ile ambayo inaletwa wakati kesi inaendelea. Moja ya sifa ya ‘DISPOSAL ORDER’ ni kwamba inatakiwa ifanyike kwa uwazi na itoke kwa namna ile ile. Kwa kesi yetu, kwa kuwa kielelezo kilipokelewa kwa Jaji, basi ni kwa namna ile ile walipaswa wamwombe Jaji yule yule au Jaji aliyerithi.

KIBATALA: Tunatambua kwamba wenzetu kupitia shahidi wa pili wamejitahidi ku- lay foundation kwamba kielelezo hicho kimetoka kwenye Mahakama. Hata kama tukisema barua iliyotoka ni authentic, basi Naibu Msajili hakuwa na mamlaka hayo with due respect. Tulitakiwa kabla ya shahidi huyu kutoa Exhibit Register_walitakiwa kutoa hapa mahakamani kupitia kwa _Exhibit Register.

KIBATALA: Hilo ni suala la kisera la Mahakama Kuu. Tulitakiwa kabla ya shahidi huyu kutoa Exhibit Register walitakiwa kutoa hapa mahakamani kupitia kwa Exhibit Register. Naomba kukurejesha kwenye nyaraka ya ‘EXHIBIT GUIDE LINES SEPTEMBER 2020’ iliyotolewa na Jaji Juma katika ukurasa wa 19 sehemu 4:3 Heading Disposal or Exhibit.

(Kibatala anasoma sehemu hiyo kwa Kiingereza)

KIBATALA: Hili ni hitaji la nyaraka ya kisera, na maelezo haya ya Jaji Mkuu hayahitaji maneno ya nyongeza.

KIBATALA: Ilikuwa ni sharti la lazima la sera la nyaraka hii yafuatwe kabla haijafika kwa shahidi na kabla haijafika kwa shahidi. Kuhusu pingamizi hili tunaomba tuishie hapa, kwamba Mahakama ikatae. Mheshimiwa Jaji, hii nyaraka ipo inapatikana ila kwa uhusiano wa kaka na dada nawaazima ya kwangu. Mheshimiwa Jaji sasa niende kwenye dhana ya ‘Estoppel’.

KIBATALA: Naialika mahakama katika kesi ya Issa Athumani vs Jamhuri ukusara wa 25 na 26, paragraph ya pili. Ilikuwa ni kesi ya madai lakini Mahakama ya Rufaa ikasema inafaa kutumika kwa kesi ya jinai.

KIBATALA: Naomba pia nikupeleke kwenye kesi namba 264 mwaka 2004 chini ya aliyekuwa Jaji Mkuu wakati huo, Jaji Othuman, Julius Michael and Four Others vs Republic katika ukusara wa sita, ukurasa wa 6, 7, 8 na 9.

(Kibatala anasoma).

KIBATALA: Kwamba jambo lililokuwa limeshaamriwa katika kesi hiyo kurudishwa tena Mahakamani mahakama imekataza. Page ya 8 ya kesi ya Julius Michael ilisema kwamba issue ya Estoppel ina maana kwamba siyo sahihi kwa jambo lililokuwa limeamriwa kurudishwa mahakamani kwa sababu ya _criminal fairness, value za taasisi zinazofanya maamuzi kulinda hadhi yake, na kutokutumia muda na fedha kuamua jambo hilohilo. Kwa kuwa jambo lilishaamriwa basi haliwezi kurudiwa tena.

Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Kibatala anakaa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji ataanza Mr Chavula.

WAKILI WA SERIKALI: (Abdallah Chavula) Mheshimiwa Jaji, kwa heshima zote baada ya kusikiliza hoja za wWenzetu ambazo zimejielekeza maeneo matatu … Hoja ya kwanza ikijieleleza kwenye kifungu cha 353(3) cha Sura ya 20 na kwamba suala zima lililopo ni dhana ya utunzaji wa kielelezo, yaani Chain of Custody. Na eneo la pili lilijielekeza kwenye kanuni inayoifunga mikono mahakama kufanya maamuzi juu ya kile ilichokiamua hapo awali.

WAKILI WA SERIKALI: Na eneo hili linaenda kihisa mamlaka ya Mahakama kuhusu kukisikiliza au kukitolea maamuzi. Kwa lugha nyingine wenzetu kwemye kanuni ya Issue Estoppel kwamba kanuni hii inakubana siyo upande wa mashitaka. Kwa heshima zote Mheshimiwa Jaji hoja zote zilizotolewa na wenzetu kwenye hoja hizo tatu hatukubaliani nazo.

WAKILI WA SERIKALI: Na ni maoni hatukubaliani nazo zote. Zinakosa miguu ya kusimama. Mheshimiwa Jaji katika kujibu nitaomba nianze na utangulizi ufuatao.

WAKILI WA SERIKALI: Siye hatuelewi ilikuwa kwa bahati mbaya au kwa makusudi, wanaipotosha Mahakama. WAKILI WA SERIKALI: Lini Mahakama hii ilifanya maamuzi kuhusu Detention Register ambayo inaombwa na shahidi? Sisi kwa pamoja tunasema HAPANA.

WAKILI WA SERIKALI: Hakuna wakati wenzetu wakisikika waliweka pingamizi dhidi ya hii nyaraka tunayotaka kuitoa na hakuna uamuzi ulifanywa na Mahakama dhidi ya hii nyaraka tunayotaka kuitoa. Kilichoamriwa ni shahidi yule wa Kwanza alishindwa kuweka misingi juu ya kielelezo kilikuwa wapi na kilifika fika vipi Mahakamani na hizo ndiyo zilikuwa hoja zilizotolewa na kubishaniwa. Hapakukuwa na shaka hiyo kwamba hicho siyo chenyewe, chenyewe kimechezewa.

WAKILI WA SERIKALI: Na hata leo hii hakuna hoja hata moja kwamba kielelezo hiki sicho alichokitoa Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, siyo katika shauri la awali wala sasa palipotolewa hoja kwamba kielelezo hicho ni irrelevant na siyo material. Mheshimiwa Jaji ulichokifanya uamuzi mara ya kwanza ulikuwa dhidi shahidi mwenyewe na siyo hiki kielelezo. Mheshimiwa Jaji, kwenye maamuzi yako tunaomba tukurejee, kwamba shahidi amekidhi vigezo vya relevance, na suala lenyewe alishindwa ku- establish Chain of Custody.

WAKILI WA SERIKALI: Hakuna mahala ulisema kielelezo hiki kadha wa kadhaa … Mheshimiwa Jaji, wanalolisema halipo wala mahakama haijawahi kulifanya. Mheshimiwa Jaj,i tunakubaliana na wenzetu kwamba ni kweli vigezo vya upokelewaji wa vielelezo ni vile vitatu, Relevance, Competence na Materiality, na kweli wakati PW1 anatoa ushahidi wake na sisi tunatoa hoja zetu, tulisema sisi Mheshimiwa Jaji tunatofautiama na wenzetu kwa namna wanavyotaka Mahakama iamini kwenye hilo eneo.

WAKILI WA SERIKALI: Kilichopo Mheshimiwa Jaji siyo vigezo. Kinachoangaliwa ni dhumuni, kwamba kielelezo kile kilipaswa kutolewa. Siye haturuhusiwi kupeleka Mahakama huko na Mahakama hatakiwi kufanya maamuzi hayo. Mahakama ilitakiwa kwa ajili ya utambuzi. Katika mahakama zetu exhibit zilizokuwa zimetolewa kwa Exhibit Purpose Mahakama haiwezi kuchukua na kufanya maamuzi yake.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kwa mantiki hiyo utaona hata mazingira ya PW1 na PW2. Hata kama Mahakama ingefanya maamuzi sisi hatufungwi. Mheshimiwa Jaji, nielekeze kwenye sheria kesi za wenzetu walizosoma.

WAKILI WA SERIKALI: Sisi tunaomba tuipeleke Mahakama mbali zaidi. Ni mazingira yapi Mahakama inaweza kukumbwa na hali hiyo ni kwenye shauri la NIBUO COSMAS vs JAMHURI, shauri la jinai namba 519 ya mwaka 2016 Mahakama ya Rufaa. Naomba kusoma ukurasa wa saba mpaka ukurasa wa nane na wa mwisho … Samahani Mheshimiwa, kuanzia mstari wa pili aya ya mwisho.

(Wakili Chavula anasoma).

WAKILI WA SERIKALI: Katika kesi yetu hakuna verdict mpaka sasa hizo authority … Kwa sasa kesi hii na kesi ambazo wemeilekeza Mahakama haina msaada kwao.

JAJI: Ukisema mamlaka unamaanisha nini?

WAKILI WA SERIKALI: Wameilekeza Mahakama katika kesi ya NBC Ltd, wakasema ni paragraph ya mwisho aya ya saba.

(Wakili wa Serikali anasoma)

JAJI: Ukurasaa wa ngapi?

WAKILI WA SERIKALI: Ukurasa wa kumi.

(Wakili wa Serikali anasoma).

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kilichopo hapa awali ilikuwa hoja, kilichopo kinafungwa muda.

(Anasoma tena ukurasa wa saba).

WAKILI WA SERIKALI: Tofauti na hapa Mheshimiwa Jaji, kilichokuwepo ni kutoa utambuzi. Na Mahakama haikualikwa kufanya maamuzi dhidi ya kielelezo chenyewe. Hivi sasa Mahakama inaalikwa kwa kutolewa kwa kielelezo. Vitu viwili tofauti kabisa. Kwa hiyo Mahakama mikono yake haifungwi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, vilevile wenzetu waliialika Mahakama hii kwenye mashauri mawili. _ISSA ATHUMAN vs JAMHURI wakaielekeza ukurasa wa 25 mpaka 26. Ukurasa wa 25 na ukurasa wa 26 Mahakama ilikuwa ikijadili uwezo wa matumizi ya kanuni hii. Hivyo Mheshimiwa Jaji ukienda kwenye huo ukurasa, miye naona … Sasa Mheshimiwa Jaji kuisaidia Mahakama yako na wengine kuelewa haya masuala naomba nielekeze kuanzia ukurasa wa saba.

(Wakili wa Serikali bado anasoma)

WAKILI WA SERIKALI: Cha kwanza lazima pawe na kesi mbili. Na moja lazima liwe limetangulia.

(Anasoma tena).

WAKILI WA SERIKALI: Sasa Mheshimiwa Jaji mie mwenzangu tunajiuliza hivi haya masuala ni mawili tofauti? Kwenye hicho kitendawili jibu ni HAPANA.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji pia walielekeza Mahakama kwenye shauri la JULIUS MICHAEL and FOUR OTHERS Vs REPUBLIC wakasema ukurasa 6, 7, 8, na 9. Miye naomba nielekeze Mahakama kwenye ukurasa wa 9. Walichozungumza ukurasa wa 6 mpaka wa nane wanafunga mkono niliyoyatoa.

(Anasoma ukurasa wa tisa).

WAKILI WA SERIKALI: Wanaunga mkono. Kwa hiyo hata hizi mamlaka za sheria walizoleta ili kuongeza nguvu kwenye hoja zao bado nazo haziwakubali. Kwa sababu hizo mamlaka mbili zimewakataa, … na siyo sahihi kwamba kanuni ya Issue Estoppel inaifunga Mahakama. Hapana! Inatufunga sisi watu wa prosecution.

WAKILI WA SERIKALI: Siye tunasema katika mazingira yote hakuna mahala wala mazigira yoyote mahakama ilishafanyia kazi. Na tunaomba Mahakama itupilie mbali mapingamizi yao kwa sababu yamekosa nguvu kisheria. Mheshimiwa Jaji nielekeze katika hoja ya kwanza.

WAKILI WA SERIKALI: Katika kuzungumza hoja yao wakazungumzia Exhibit Guidelines. Anyway. Nisizungumze sana kuhusu hizo guidelines.

WAKILI WA SERIKALI: Wanataka kutenganisha Trial Within a Trial iliyofanyika kwa mshitakiwa wa pili na shauri hili kubwa la kesi namba 16 ya mwaka 2021, kwamba ni vitu viwili tofauti na kwamba havitegemeani. Na hata kinachofanyika sasa ni ku- separate Trial Within Trial.

WAKILI WA SERIKALI: Hatuwezi kuvitenganisha hivi. Vinaemda sambamba mpaka Mahamaka siku inatoa hukumu ya kuwaachia washitakiwa au kuwatia hatiani. Ya leo ni procedure tu ya ku- admit tu kielelezo. Na effect yake haiendi ku- dispose kesi ya Uhujumu Uchumi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, utaratibu huu kwa sababu ni utaratibu wa kipekee ndiyo kunahitajika kuwe na ushahidi ndiyo kielelezo kiingizwe.

WAKILI WA SERIKALI: Trial Within a Trial ni process tu ya admissibility. Sasa Mheshimiwa Jaji sote tunafahamu kwamba Mahakama ili itoe amri lazima kuwe na maombi. Na hayo maombi hayo … Maombi yote yanaongozwa na kifungu namba 394 (a) Sura ya 20 ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, na kwamba maombi yanaweza kufanywa kwa maandishi au kwa mdomo.

WAKILI WA SERIKALI: Subsect inasema kwa wito au kiapo cha Mahakama. Mheshimiwa Jaji, wenzetu wanataka kuleta Chamber Summons au la tulete maombi yetu kwa njia ya mdomo. Haiwezekani kwa sababu asili ya maombi yako yataonyesha umeyaleta kwa ombi gani. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji namna pekee Iliyobakia tukienda na hiyo leading ilikuwa ni kuomba kwa njia ya mdomo.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati PW1 anatoa ushahidi wake tulitoa hoja na hoja hiyo ilitolewa na baada ya maombi hayo mahakama ikatoa maelekezo kielelezo hicho kitolewe, nasi tukakabidhiwa. Wakati tunakabidhiwa wenzetu hawakupinga kwamba haya maombi siyo, badala yake walikaa kimya.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati tunakitoa ndiyo wakaanza kuweka mapingamizi. Wenzetu wakasema hawa mabwana kuna kitu walitakiwa wafanye. Mheshimiwa Jaji, utaratibu ule tulioufanya wenzetu waliupinga.

WAKILI WA SERIKALI: Kwamba tulitakiwa tupate ‘0rder’ kwa sababu lile kabrasha lilishafungwa na likawekwa stoo. Sasa wanatuchanganya wenzetu.

WAKILI WA SERIKALI: Tumefuata maelekezo ya Mahakama wenzetu wanasema hakuwa sahihi lazima ipatikane amri.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji hapa sasa lazima ieleweke na lazima tuelewane. Wenzetu watuelewe nini tunachokitaka sisi.

WAKILI WA SERIKALI: Sisi tunatambua hiki kifungu cha 353 ambacho kinapatikana sehemu E ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambapo pale kuna kichwa cha habari kinasomeka Disposal of Exhibits. Mheshimiwa Jaji na sisi tunatambua kweli kwamba lazima Mahakama itoe amri yake. Lazima kuwe na amri ya mahakama.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa minajili ya kifungu cha 353(1) kifungu kinatoa mwongozo kwa Mahakama. Je, ni wakati wa kufanya amri ya kufanya disposal ya kielelezo? Kifungu hiki Mahakama itakitumia pale tu ambapo kielelezo kimetolewa Mahakamani na Mahakama ikakipokea kama ushahidi. Na baada ya kukipokea shauri hilo limeenda hadi mwisho Mahakama ikalikamilisha.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji shauri limeisha. Hakuna mtu anayemmiliki kielelezo kile na hakuna mtu anayekuja kudai kielelezo kile Mahakamani na hakuna rufaa iliyokatwa hapo ndipo Mahakama itatoa amri ya kufanya disposal. Kumekosekana na basi hakuna namna basi Mahakama lazima iangalie namna ya kuki- dispose hicho kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kwenye shauri letu hali ni tofauti. Sisi hatujaomba kielelezo hicho kiende kukaa kwa mmiliki wa kielelezo.Hapana. Hatujaomba hivyo. Exhibit P1 kwenda kwa Msajili wa Mahakama, yaani barua.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi ameonyesha lengo lake ni kutolea ushahidi. Hoja ya kwamba sisi hatujapaswa kukidhi vigezo kwa mujibu wa kifungu cha 353 sisi tunasema HAPANA.

WAKILI WA SERIKALI: Ingekuwa shauri hili ni tofauti ingekuwa sawa. Lakini sasa shauri ni moja na tunachokitumia kipo ndani ya kesi moja hiyo hiyo. Na hata ukiangalia mwongozo wa wenzetu kipengele cha nne na cha tatu ‘Disposal of Exhibit is done at the end’.

(Anasoma tena yote)

WAKILI WA SERIKALI: Under special circumstances disposal can be done before or during the trial. Sasa Mheshimiwa Jaji wenzetu walitakiwa waeleze sasa hizo special circumstances zilizotakiwa zifuatwe. Sisi tuna kazi kwamba huwezi kutengenisha Trial Within a Trial na shauri namba 16 la mwaka 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji hoja yetu siye tumekiomba kielelezo ili tukitumie kwenye proceedings hizi hizi na tumekileta tukitumie kwenye proceedings hizi hizi. Sisi tunasema siyo kifungu cha 353 wala mwongozo wa Mahakama ukurasa wa 19.4:3 unaweza kutumika kwa sababu mazingira tofauti.

WAKILI WA SERIKALI: Na hoja ya wenzetu ni kwamba kielelezo kimepatikama illegally.

JAJI: Mh!

MTOBESYA: Hapana! Hapana!

WAKILI WA SERIKALI: Basi niweke hivi kimekiuka kifungu cha 353. Namaliza kwa kusema hakuna kilichokiukwa. Naomba niwakaribishe wenzangu.

(Wakili wa Serikali Pius Hilla anasimama)

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa, kwanza naunga mkono aliyoyaongea wakili msomi Chavula. Lakini submission yangu itaendana na kesi ya ABASI KONDO vs JAMHURI Criminal Appeal namba 472 ya mwaka 2017 Mahakama Kuu ya Dar es Salaam. Mheshimiwa Jaji, katika shauri hili Mahakama ya Rufani ilisema kwamba Oral evidence is sufficient without … Kwamba “where a fact is submitted orally, it does not need documents to prove that facts.” Mheshimiwa Jaji, submission za utetezi ukiangalia kwa maana yake sababu kubwa zimejikita kwenye Chain of Custody. Mheshimiwa Jaji tayari ipo kwenye rekodi za Mahakama kupitia ushahidi namna gani kielelezo kilivyofika Mahakamani, kilivyoombwa na hadi kinaletwa Mhakamani. Hakuna mahala Mahakama yako imeelezwa kwamba ushahidi huo hauna maana.

WAKILI WA SERIKALI: Na haijafika mahala kusema kwamba shahidi ambaye ameeleza hayo is relevant. Hakuna kifungu kinasema kwamba disposal ya kielelezo ni kwa amri ya Mahakama. Sisi ni wasilisho letu kwamba administration ni njia mojawapo ambayo shughuli inaweza …

JAJI: Hujamalizia.

WAKILI WA SERIKALI: …Kwamba shughuli inaweza kupatikana hata kwenye utawala.

WAKILI WA SERIKALI: Kwamba ni wasilisho letu kwamba kielelezo kimetoka kwenye mikono ya Mahakama. Mheshimiwa kwamba ilitakiwa Exhibit Register ilitakiwa ionyeshe kwamba la! la! la! … hatuoni umuhimu wa hilo. Walikuwa wanazungumzia kuhusu mwongozo wa Mheshimiwa Jaji Mkuu. Hatupo nao mbali sana.

WAKILI WA SERIKALI: Lakini ‘page one’ ya mwoongozo ‘paragraph’ ya kwanza mstari wa kwanza unasema …,

(Wakili wa Serikali anasoma).

WAKILI WA SERIKALI: Zinatakiwa kusomwa na sheria zinginezo. Sheria ya kesi na nyaraka zingine za Mahakama. WAKILI WA SERIKALI: Zinatakiwa kusomwa na sheria zinginezo. Sheria ya kesi na nyaraka zingine za Mahakama. Mheshimiwa Jaji imekuwa submitted pia kwamba Detention Register ina mapumgufu ya kisheria ndiyo maana ilikataliwa hivyo haiwezi kuletwa tena. Na kwamba Litigation must come to the end. Bila kutumia maneno mengi Mheshimiwa Jaji ambayo ni _subject matter ya submission yetu, hakuna mahala imekuwa declared kwamba siyo competent kwenye procedure zaidi ya kwamba ilikuwa ni suala la shahidi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, hoja ya kwamba Mahakama ipo ‘funtus officio’ kwa kutumia kielelezo hiki, siyo sahihi. Hakuna element ya relitigation kwa kuwa kielelezo hicho kilikuwa competence na pia purpose haikuwa hiyo. Ni submission yetu Mheshimiwa kwamba hakuna decision ambayo ime- decide Detention Register isipokelewe.

JAJI: Nakukumbusha ulisema utazungumza kwa kifupi sana.

JAJI: Sasa umeshatumia nusu saa.

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Mheshimiwa naomba nimalizie tu kesho.

JAJI: Naomba kuahirisha shauri hili mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Jaji anaandika).

JAJI: Shahidi utarudi tena kizimbani kesho regardless ya kitakachotokea. Washitakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho asubuhi saa tatu. Nawatakia jioni njema.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama.

https://sautikubwa.org/kesi-ya-mbowe-jaji-tiganga-atoa-uamuzi-wenye-ukakasi-aahirisha-kesi-mara-tatu/


No comments :

Post a Comment