Diaspora Digital Hub Tarehe 22 Mei, 2023 Saa Nne Kamili Asubuhi Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itazindua Mfumo wa Kuwasajili Kidigitali Diaspora wote wenye asili ya Tanzania. Kama sote tunavyofahamu, nchi nyingi duniani zimekuwa na utaratibu wa kuwahesabu na kuwasajiri kidigitali Diaspora wao, ili kuziwezesha Serikali kuandaa na kutekeleza mikakati mbalimbali muhimu kwa mustakabali wa Diaspora wao na maendeleo ya nchi. Kumbe, ni vema na sisi Diaspora wa Tanzania tujitokeze kwa wingi kujisajili Mfumo utakapozinduliwa. Naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuchukua hatua hii ya kutusajili kidigitali badala ya ule utaratibu wa zamani wa kujiandikisha kwenye Madaftari Ubalozini.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
No comments :
Post a Comment