dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 5, 2024

President Ruto Announces Austerity Measures to Compensate for Loss of Re...!


Rais wa Kenya, William Ruto ameondoa bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ofisi ya Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Kiongozi na amefuta Mashirika 47 ya Serikali na kusitisha safari zisizo za lazima kwa Wafanyakazi wa Serikali pamoja na kuzuia ununuzi wa magari mapya ya Serikali.

Akihutubia Taifa la Kenya leo July 05,2024 Ruto ametangaza kupunguza idadi ya Washauri wake kwa 50% ambapo ameanzisha hatua nyingine kadhaa za kubana matumizi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inaingia na pia amekata bajeti za ukarabati wa majengo ya Serikali kwa 50%.

Ruto pia amesema hakuna Afisa wa Serikali atakayeruhusiwa kushiriki katika shughuli za kuchangisha pesa zinazoendelea na amewaagiza Maafisa wa Serikali kuacha shughuli za hisani, hasa walioonekana wakionyesha pesa nyingi wakati wa hafla za kutoa misaada ambayo imezua taharuki kutoka kwa Wakenya.

Ruto amesema kufuatia mashauriano mapana na wenzake wameafikiana kupunguza gharama mbalimbali zikiwemo kufuta angalau Mashirika 47 ya Serikali yenye vipengele vinavyoingiliana lengo likiwa ni kuboresha huduma za Serikali kwa Wananchi na kuwafanya Wakenya wapate huduma sahihi kutoka Serikalini.

No comments :

Post a Comment