dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 12, 2024

ZACADIA YAIFADHILI BBQ YA WATOTO WA TORONTO!

ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) ni Jumuiya ambayo ni kiungo baina ya wale wote wenye asili ya Zanzibar wanaoishi Canada na Zanzibar.
Zacadia imeamua Summer hii kuifadhili BBQ ya watoto wa chuoni wa Madrasa ya Abu-Ubaydah Islamic Centre ya mjini Toronto pamoja na wazee wao.

BBQ hii itafanyika siku ya Jumamosi tarehe 17 August, 2024 katika park ya Northwood Park, North York, Toronto.

Blog hili lilimtafuta Makamu wa Rais na Mshika Fedha Mkuu wa Zacadia Nd. Hassan Othman na tulipompata tukamuuliza nini hasa ilikuwa nia ya Jumuiya ya Zacadia kuifadhili hii BBQ, nae alitujibu kuwa..." Nia kubwa ni kuwafurahisha watoto wetu hasa katika msimu huu wa Summer wakati wanapumzika majumbani na wazee wao, lakini zaidi tunataka kuchukuwa nafasi hii kukutana na wazee wao ili kuwajulisha mambo mazuri mazuri yanayotokea kwenye Idara ya Diaspora kule nyumbani Zanzibar".

Tulipomuuliza Nd. Othman ni mambo gani hayo mazuri mazuri yanayotokea kule nyumbani Zanzibar kwenye Idara ya Diaspora, yeye alijibu..." Siku nyingi sisi tuliokuwa huku nje tulikuwa tukitaka tutambulike nyumbani, sasa tunatambulika. Na sio tunatambulika tu bali sisi sote tunaoishi nje na ambao tunaasili ya Zanzibar tutapatiwa vitambulisho maalumu kwa kila atakaejisajili. Vitambulisho hivi vitatuwezesha kufaidika  na mambo tele, kama vile:
  • Kusamehewa kibali cha kazi
  • Kurahisishiwa kwa Wana-Diaspora kwenye mambo ya ardhi.
  • Kibali cha ukaazi kupatikana kwa wepesi na haraka  (ambacho kitakuja kuchukuwa nafasi ya Hadhi Maalumu (Special Status) pale itakapomalizika mchakato wake ambao tayari ushaanza Bara na Visiwani
  • Kamisheni ya Utalii na Kamisheni ya Uwekezaji (ZIPA) kufanya utaratibu kwa Wana-Diaspora wanaowekeza kuwa bila ya pingamizi.
  • Kuondolewa kwa malipo ya ticket kwa pesa za kigeni kwa Wana-Diaspora wanaposafiri baina ya Unguja, Pemba na Dar Es Salaam.
Kwa ufupi, faida ni nyingi na siwezi kuzimaliza kwa kuzitaja zote hapa", alielezea Nd. Othman.

Akiendelea, Nd. Othman alisema kwamba yote haya na zaidi atayapata Mwana-Diaspora kutoka Zanzibar atakaejiandikisha kwenye website ya Zanzibar Diaspora. Akimaliza Mwana-Diaspora kujiandikisha atapata hapo hapo ID namba yake ya kitambulisho atakachokipata na ataweza kujiunga na kikundi cha Wazanzibari ambao tayari washajiandikisha na wanangojea kadi zao.

Ili kujiandikisha Nd. Othman alitujulisha kwamba inabidi utembelee tovuti la Zanzibar Diaspora  lenye address hii hapa chini:


Na kama mtu atapata matatizo yoyote yale katika kujiandikisha basi apeleke tatizo lake hapa:

BBQ hii ya watoto na wazee wao inategemewa kuanza saa 6 mchana mpaka saa moja za usiku.

Nd. Othman alilieleza blog hili kuwa pia Zacadia itawajulisha wote watakaohudhuria hii BBQ kuwa imeiomba benki yetu ya Watu Wa Zanzibar (PBZ LTD) kuwafanyia wepesi wote wale wanaotaka kufunguwa akaunti nyumbani, kama vile kuondoa ada ya kila mwezi - kama wanavyofanya benki nyengine za nyumbani.

"Tulishawaomba wenzetu wa benki yetu ya PBZ Ltd na hili suala wanalifanyia kazi hivi sasa", aliendelea Nd. Othman na akamalizia kwa kusema kwamba..."Ni muhimu tuweke viakiba vyetu nyumbani hasa baada ya somo tunalolisoma hivi sasa kutokana na ghasia zinazoendelea kule Uingereza dhidi ya wahamiaji, ghasia ambazo zinaweza zikatokea katika nchi yoyote ile tunayoishi huku nje, kwahivyo tusikusahau kwetu, after all, MTU KWAO NDIO NGAO", alimalizia Nd. Othman.

Pia bonyeza hapa kwa maelezo zaidi:

No comments :

Post a Comment