POLEPOLE NI NYANI ASIYEONA KUNDULE
1. Katika barua yake ya kujiuzulu aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na mambo mengine analaumu au kushutumu kuhusu watu kupotea.
Kinachonitatiza ni kwamba kwani wakati yeye akikitumikia chama na serikali watu hawakupotea? Alijibu nini juu ya hilo?
Kwani Azory na Benny hawakupotea yeye akiwa kwenye chama na akiwa kiongozi serikalini? Serikali imekuwa ikipambana na uhalifu wote kupitia vyombo vyake vya ulinzi.
2. Amegusia demokrasia akilaumu kinachoendelea nchini na ndani ya CCM.
Je, akiwa kiongozi ndani ya chama na serikali vyama pinzani havikuzuiwa kufanya siasa? Alisema nini zaidi ya kujivunia hatua hiyo?
3. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni Rais muungwana sana Watanzania tumejaliwa kuwa naye.
Rais amefungulia siasa na watu kusema. Vyama vya siasa vinafanya siasa tofauti na wakati yeye akiwa na mamlaka.
Rais ameahidi hadharani kuwa mchakato wa Katiba utaendelea kati ya mwakani na 2030, kilio cha upinzani ambacho mtangilizi wake alisema hakikuwa kipaumbele chake!
Kuhusu ustawi wa Watumishi wa Umma, Rais amepandisha kiwango cha chini cha mshahara jambo ambalo halikufayika miaka sita mfululizo kabla yeye kuongoza nchi.
Tukumbuke kuwa ni Rais Dkt Samia ndiye aliyekwenda Nairobi kumuona Tundu Lissu ilihali kila mtu alihofia kufanya hivyo na kila mmoja alikuwa na sababu zake.
Alipoapishwa Rais alikuja na falsafa ya R4 ambazo kila mtu kazitumia kufanya mambo yake kwa Uhuru.
4. Amelaumu demokrasia ndani ya CCM.
Ninakumbuka Wajumbe wa Kamati Kuu walipunguzwa kutoka 34 hadi 24 wakati wa Utawala wa awamu ya tano.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu walipunguzwa kutoka 388 hadi 158. Hiyo haikuwa dosari? Mbona mengi yalisemwa na yeye hakujibu neno?
Mwaka 2020 kwenye mchujo wa watia nia kulikuwa na jambo jipya. Wengi walioshika nafasi ya kwanza na pili waliachwa wakachukuliwa waliokuwa wa tatu hata wa nne. Hii haikuwa dosari?
5. Turejee kidogo uchapakazi wa Rais Dkt Samia na hitimisho la andiko langu.
Rais Dkt Samia alipokea miradi ya kimkakati takribani 16 ikiwa michanga na ameitekeleza kwa haraka na sasa matoleo tunayaona.
Nina wasiwasi kuwa Polepole anayo agenda yake ya siri na hataki kuisema. Atueleze Watanzania ni nini agenda yake.
RAIS SAMIA TUPO NAE NA TUNATAMBA NAWE HADI 2030.
Suphian Juma Nkuwi,
Kada-CCM
No comments :
Post a Comment